Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakiwekwa sokoni tu, wanauzika fasta

Realclatouschama Wakiwekwa sokoni tu, wanauzika fasta

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha dogo la usajili linaendelea tangu lilipofunguliwa Desemba 16 mwaka jana. Baadhi ya timu zipo Visiwani Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na huko zinasaka wachezaji wa kuwasajili.

Yanga, Simba na Azam FC tayari zimeanza usajili na Yanga imemshusha Augustine Okrah kutoka Bechem United na Shekhan Ibrahim (JKU) hadi sasa, Simba imemsajili Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar), Salehe Karabaka (JKU), JKT Tanzania Shiza Kichuya (Namungo) na Azam FC, Mohamed Mustafa (El Merreikh), Franklin Navarro kutoka Cortulua FC ya Colombia hao ni baadhi tu.

Kuna wachezaji hao, viwango vyao vinaongeza utamu kwenye madirisha ya usajili na vigogo hupambana kunasa saini zao kama ikitokea wakawekwa sokoni.

Mwanaspoti linakuchambulia baadhi ya mastaa ambao viwango vyao kwa sasa vipo juu na ikitokea dirisha hili au lijalo wakawekwa sokoni, itakuwa hapatoshi na mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama.

AZIZI KI - YANGA

Kwa sasa ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akiwa nayo 10 na zaidi nane kati ya hayo amefunga kwa guu lake la dhahabu la kushoto na asisti tatu.

Ubora wake umemfanya awe anaitwa mara kwa mara timu ya taifa na hivyo, kumweka sokoni ni dili kubwa kwani anazitamanisha timu kibao.

Mkataba wake unaisha mwisho wa msimu na Yanga kama inataka kuendelea naye itabidi ipambane kumbakisha au ichukue pesa ndefu kwa klabu nyingine inayomtaka.

CHAMA - SIMBA

Kiungo matata ambaye kwa sasa ana mgogoro na timu yake na amesimamishwa kwa muda.

Hata hivyo, kwa makubwa aliyofanya akiwa na Simba licha ya utuvu wa nidhamu alioonyesha, akiwekwa sokoni dirisha hili au lijalo, atatikisa.

Hakuna asiyejua ubora wake. Amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2019/20, uliofuata (2020/21) alikuwa kinara wa asisti (tisa) na alimaliza na mabao manane.

Kama akiondoka Simba, ni rahisi sana kupata timu nchini na hata nje ya nchi. Kwa sasa yuko na timu ya taifa ya Zambia.

WAZIR JUNOR - KMC

Mshambuliaji wa KMC, Wazir Junior aliufunga vyema mwaka 2023, akifunga mabao mawili dhidi ya Simba, mchezo huo ukimalizika kwa sare ya mabao 2-2, Uwanja wa Azam Complex.

Hadi sasa mchezaji huyo anamiliki mabao saba, msimu huu amekuwa kwenye kiwango cha juu, kinachotamanisha timu pinzani kumsajili dirisha hili na hata lijalo mwishoo wa msimu.

LEY MATAMPI – COASTAL UNION

Hatajwi sana, ila kipa wa Coastal Union, Ley Matampi, amekuwa kwenye kiwango kizuri cha kuisaidia timu yake. Ndiye kinara wa kutokuruhusu mabao (clean sheet) akiwa nazo nane.

Ingawa yuko kwenye moja ya timu kubwa nchini, lakini akitakiwa na timu nyingine yenye masilahi zaidi ni rahisi kutokana na ubora wake alioonyesha msimu huu hadi sasa.

KIPRE JUNIOR - AZAM FC

Azam ina mtu kweli. Azam ina pesa. Inashusha vyuma lakini kwa Kipre, imeotea kweli. Ana kiwango kikubwa kwa sasa akisaidia timu hiyo kuwa kinara kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa kiwango chake hicho, hata miamba ya soka nchini Simba na Yanga zinammezea mate, achana na ofa zitakazokuja kutoka nje.

Dili lake kama litatokea dirisha lijalo au hili, Azam ikiamua kumuuza, italamba pesa ndefu.

JAMES AKAMINKO – AZAM FC

Kiungo wa Azam FC, James Akaminko inaelezwa hali si shwari kwenye kikosi cha Azam. Kuna tetesi hana maelewano na kocha wake, lakini bado ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa kwenye Ligi Kuu Bara.

Kama itatokea akauzwa au kuachana na Azam, dili lake ni kubwa kwani anamezewa mate na timu kubwa ikiwamo Simba.

MAROUF TCHAKEI – SINGIDA FOUNTAIN GATE

Kiungo wa Singida United, Marouf Tchakei hadi sasa amefunga mabao matano na ameonyesha kiwango kikubwa kinachofanya Bruno Gomes kuanzia benchi, ubora wake unaweza ukazivutia timu nyingine kupeleka ofa kama si dirisha hili, basi lile kubwa lijalo. Tusubiri tuone.

FRED GIFT - YANGA

Hatajwi sana. Ni kwa sababu hapati muda mwingi wa kucheza, lakini, ana kitu na kama akipata nafasi ni beki bora. Kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi juzi dhidi ya Jamus, alionye4sha uwezo na kuchaguliwa mchezaji mwenye nidhamu. Ni wazi akiwekwa sokoni kuna timu zitammezea mate wapate huduma yake.

MOSES PHIRI - SIMBA

Ana bao moja Kombe la Mapinduzi alilofunga dhidi ya JKU. Amekuwa akitajwa sana kutakiwa na Yanga.

Kwa kiwango chake tangu asajiliwe Simba, si rahisi kukosa dili la maana na hasa timu kubwa kama Yanga inayotajwa, pia Azam na timu nyingine kubwa nje ya nchi. Anajua.

JEAN BALEKE/SAIDO

Hawa mikataba yao inaweza kufikia tamati mwisho wa msimu, lakini bado ni muhimu Simba. Hata hivyo, kwa ubora wao wakiwekwa sokoni, watasumbua na timu nyingi zitataka huduma zao.

Hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara, Jean Baleke ana mabao nane, huku Saido Ntibazonkiza akiwa na manne na hadi msimu unamalizika wanaweza wakawa na idadi kubwa zaidi na kuongeza thamani yao sokoni.

Wapo wachezaji ambao wameonyesha viwango vizuri lakini kuwapata lazima uvunje mikataba yao kwa pesa ndefu, kama Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Feisal Salim, Kibu Denis, Djigui Diarra na wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live