Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Yanga: Kipa Simba hana hadhi ya kucheza Ligi Kuu

Simon X Kipa Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amshukia Golikipa wa Simba

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa si siku mbili tu zimepita tangu Simba imtambulishe Mlinda mlango mpya raia wa Brazil Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior kuja kuziba pengo lililoachwa na Aisha Manula ambae anauguza majeraha.

Tayari Kipa huyo ameanza kuwekewa zengwe akitajwa kuwa hana sifa za kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior ametoka Ligi daraja la nne nchini Brazil na ni kinyume na kanuni za Ligi Kuu Bara.

Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika

"Kanuni ya 62 (4) - Kanuni za Ligi Kuu, Toleo la mwaka 2022 inasema;

“Mchezaji wa kigeni anayeruhusiwa kusajiliwa kwenye Ligi Kuu ni yule anayecheza katika timu ya Taifa ya nchi yake au Ligi Kuu ya nchi husika.

Mchezaji kutoka Amerika ya kusini na Ulaya, lazima awe anacheza angalau kuanzia Ligi Daraja la Tatu (Kitaifa, kutegemea mfumo kwa nchi husika).

Mazingatio ya Daraja mchezaji analocheza kabla ya usajili wake kwenye Ligi ni kwa wakati husika au kipindi kisichozidi miezi sita tokea ameachana na timu yake ya mwisho kwa mchezaji aliye huru” Mwisho wa kunukuu..

Sasa kama mchezaji katoka kwenye Ligi ya Mkoa au Ligi daraja la 4 huko Amerika ya kusini, usajili wake utakuaje hapa nchini? Naombeni kuelimishwa".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: