Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Yanga: Azam walifurahi kutufunga, sasa tunakutana

Yanga Aziz WA0007 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao dhidi ya Azam FC.

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa Yanga, Wakili Simon Patrick amesema kuwa baada ya Klabu ya Azam kushinda kwenye mchezo wao wa Ligi dhidi ya Yanga, walifurahi, sasa ni muda wa Yanga kulipa kisasi.

Wakili Simon amesema hayo baada ya Yanga kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa kuifunga Ihefu bao 1-0 jana katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana.

Yanga watakutana na Azam kwenye fainali hiyo kwa mara nyingine baada ya miamba hao kucheza fainali msimu uliopita na Yanga kuibunga mabingwa kwa bao la kennedy Musonda.

"Timu kubwa siku zote hushinda kikubwa, hongera sana jeshi la Wananchi kwa kuendelea kuleta heshima Jangwani.

"Ila fairly speaking, Ihefu ndio timu pekee hapa Tanzania imefanikiwa kuipa changamoto Yanga, walifanikiwa kuidhibiti game plan yetu.

"Kuna ka timu kalituotea kakaumiza wachezaji wetu wakati tuki focus na game ya Champions League kalifurahi kweli, sasa nasemaje, sisi ni Pipo. Champions to the final. Kibegi FC watching from home," amesema Wakili Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live