Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Simon: Hakuna mtu kupewa uraia, tutapambana wenyewe

Simon Patrick Dongo Wakili Patrick Simon.

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasheria ya Klabu ya Yanga, Simon Patrick amesema kuwa hakuna haja ya kuwapa watu wengine walioko nje uraia wa Tanzania kwa ajili ya kuja kuipambania taifa Stars badala yake wapewe nafasi wachezaji waliopo na waliofikisha timu hapo.

Wakili Patrick amesema hayo kufuatia mijadala kuibuka mitandaoni kuwa ni wasaa sasa wa Serikali kutafuta wachezaji wazawa wa Tanzania wanaocheza nje na kuwapa uraia ili kuja kuisaidia timu yao.

"Baada ya timu yetu ya taifa kufuzu michuano ya Afcon 2023, kumekua na mijadala mbali mbali juu ya wachezaji wenye asili ya Kitanzania waliobadilisha uraia kutafutwa ili waipambanie nchi.

"Japo ni hoja nzuri, mimi nimekua na mtazamo tofauti. Yaani watu wapambane kivyao na wafanikiwe bila msaada wowote, then tuanze kuhangaika kuwaomba waje wachezee Taifa Stars!?

"Kwangu hii sio sawa, ifike mahali Watanzania tujenge desturi ya kuvuna tulichokipanda sio kupenda njia za mkato.

"Viongozi wetu wakiamua kuzinduka usingizini, wanauwezo mkubwa wa kutengeneza kizazi cha wachezaji wenye uwezo wa kutupeleka mbali kwenye mafanikio ya kisoka, ni vile tu hatupendi kujifunza mambo mazuri kwa waliotuzidi.

"Tuwaache vijana walioamua kutafuta maisha sehemu nyingine waendelee kufurahia matunda ya juhudi zao, tusiwasumbue. Tutengeneze wachezaji wetu, na tusiwakatishe tamaa wanajeshi wetu waliopambana mpaka tukafuzu Afcon ya mwaka 2024.

"Uraia pacha sio suluhisho la matatizo yetu kwenye mpira, hakuna mchezaji mzuri atakayepata namba kwenye timu ya taifa kubwa akaacha fursa hiyo akaja kuichezea Tanzania.

"The seeds you plant today, are the fruits you’ll reap tomorrow," amesema Wakili Patrick Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: