Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakali watano wa mabao Afrika

ASAMOAH GYAN Wakali watano wa mabao Afrika

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna magwiji wa soka kutoka bara la Afrika, ambao wamekuwa wakishiriki fainali za Kombe la Dunia kwa miaka kadhaa, na zaidi watapata nafasi kuandika majina yao katika vitabu vya kihistoria huko Qatar baadae mwezi huu.

Hapa tunaangalia wachezaji watano waliofunga mabao mengi kutoka Afrika katika fainali za Kombe la Dunia.

5. PAPA BOUBA DIOP (SENEGAL) – Mabao 3 Kiungo Diop aling’ara baada ya kufunga bao la kwanza katika Kombe la Dunia mwaka 2002 huko Korea Kusini na Japan, akiisaidia Senegal kuwafunga mabingwa watetezi Ufaransa kwa bao 1-0. Alifunga mabao mawili zaidi dhidi ya Uruguay wakati timu hiyo ya Afrika Magharibi ikitinga robo fainali katika mashindano yake ya kwanza na Diop alimaliza akiwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao matatu.

4. SAMUEL ETO’O (CAMEROON) – Mabao 3 Kwa sasa ndiye Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon, ambaye wakati wa kipindi chake cha uchezaji alifanya vizuri. Alichaguliwa katika fainali nne za mashindano hayo, akiwemo mchezaji chipukizi katika fainali za Ufaransa mwaka 1998 wakati akiwa na umri wa miaka 17 tu, kwa ujumla akicheza mara nane.

3. AHMED MUSA (NIGERIA) – Mabao 4 Musa alifunga mabao 16 katika mechi 107 wakati akiichezea Super Eagles, lakini mabao manne yalipatikama katika fainali za Kombe la Dunia. Aliichezea Super Eagles katika fainali mbili zilizopita lakini ameshindwa kurudi tena baada ya Super Eagles kushindwa kufuzu kwa fainali za mwaka huu nchini Qatar.

2. ROGER MILLA (CAMEROON) – Mabao 5

Milla ni mchezaji mkongwe zaidi kuwahi kufunga katika fainali za Kombe la Dunia baada ya kupachika bao dhidi ya Russia mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 42, ambao pia likiwa ni bao lake la mwisho kati ya matano aliyofunga. Alicheza katika fainali za mwaka 1982 na alifanikiwa kucheza mechi zote tatu za hatua ya makundi akiwa na Simba wasiofungika bila ya kufunga bao lolote, lakini mwaka 1990 alifanya mambo makubwa.

1. ASAMOAH GYAN (GHANA) – Mabao 6 Ndiye anayeshikilia rekodi, ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, ambaye alifunga bao lake la sita na kusaidia mara tatu katika mechi 11 alizocheza katika mashindano mawili kati ya mwaka 2006 na 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live