Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakala wa Ben White awakosoa wakosoaji

Ben White Msg.jpeg Wakala wa Ben White awakosoa wakosoaji

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Beki wa Arsenal Ben White, amewataka Mashabiki wa soka nchini England kumtendea wema mchezaji wake anapokuwa katika majukumu yake ndani na nje ya Uwanjani.

White aliifungia Arsenal mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi ya England, juzi Jumanne (Aprili 23), Uwanja Emirates jijini London.

Alexander Levack wakala wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26, amekiri kuwa muhanga wa shutuma anazozipata mteja wake, hasa baada ya kuchukua uamuzi wake wa kutoichezea England chini ya Kocha Mkuu Gareth Southgate.

Alexander Levack amendika katika kurasa zake wa Mitandao ya Kijamii: "Ninahisi kulazimishwa kuandika hii leo baada ya uwezo mkubwa aliounesha White katika mchezo dhidi ya Chelsea na kufunga mabao mawili,"

“Kwa muda wa majuma manne yaliyopita Ben amekuwa kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii kwa kiasi kikubwa, lakini kwa asilimia kubwa alitajwa kwa mambo mabaya pekee na wengine wakashiriki kumchafua.

"Ingawa ninashukuru kuwa Ben aliendelea kuwa mpole na kushiriki shughuli zake hadharani, jambo ambalo linaleta maana kwake na kuwaacha midomo wazi wakosoaji, nilitaka kusema kwamba huyu ni binaadamu ambaye ana hisia sawa na sisi sote.”

"Ben ameonyesha uimara na nguvu za ajabu katika kipindi hiki kigumu nje ya uwanja na amezuia kelele zote na amefanya vizuri sana uwanjani, katika hali ambayo wengine wengi wasingeweza na wangepotea kabisa.

“Ben ana tabia ya ajabu na amefanya vizuri sana uwanjani, mtazamo ambao unamruhusu kuendelea kuonesha uwezo wa kuzunguka katika maisha yake ya kazi na ya kibinafsi, nadhani ujumbe mkuu ni kuwa mkarimu kwa watu.

“Kwa upande wa Ben hatutaki kusema hadharani, na mimi sitaki kujua nini kinaendelea katika maisha ya kibinafsi ya watu kwa hivyo tafadhali tujaribu kuwa na huruma na kuheshimu maisha ya watu wengine."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live