Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakala: Napoli wanastahili kushtakiwa

Victor Osimhen Vvv Wakala: Napoli wanastahili kushtakiwa

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa mshambuliaji Victor Osimhen alithibitisha jana kuwa kitendo cha Napoli kuposti Video ya Victor Tiktok ambayo ilionesha kumzihaki na kumchafua hatokaa kimya kwa sababu hata mwaka jana Victor aliteseka na masuala ya mitandaoni pamoja na udhalilishwaji wa mchezaji huyo ambaye ilimsumbua kiakili wakala alisema...

Baada ya mda mfupi jana baada ya kuonekana video hiyo haijawafurahisha wengi uongozi wa Klabu ya napoli uliifuta mda mfupi uliofuata ambapo hadi mda huu inasemekana mambo sio shwari kati ya Napoli na Upande wa Victor!

Victor Osimhen ameshaanza kuchukua maamuzi ya kuonesha kuchukizwa na kitendo hicho ambapo yeye binafsi tayari ameshakwisha kufuta picha na video zake zote ambazo alikwisha kuchangia kwenye mtandao wa Instagram picha za yeye na klabu ya Napoli!

Inatarajiwa kufanyika mawasiliano ya kutafuta suluhu na endapo suluhu itakosekana, msimu huu mchezaji huyo raia wa Nigeria ambaye ana umri wa miaka 24 ambaye tayari msimu huu wa 2023/24 amefanikiwa kufunga magoli 3 kwenye mechi 5 za mwazo wa ligi msimu huu, vilabu vikubwa vinatajwa kuwa tayari kuchuana vikali ili kuipata huduma ya mshambuliaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live