Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahuni wamtandika mwamuzi Ligi Kuu

Mwamuzi Pic Data Mwamuzi ashambuliwa

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwamuzi Abdalla Said ameshushiwa kipigo kutoka kwa wachezaji wa timu ya Kisiwani FC na wengine wamenusuruka na kipigo hicho katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar, uliopigwa Uwanja wa Gombani timu hiyo ilipocheza na Malindi FC.

Waamuzi waliochezesha pambano hilo ni Yakob Mohamed Khalfan, Jafari Juma Chande, Abdalla Said Ali, Ibrahim Ali Ubwa mmoja akiwa kamisaa kwenye pambano hilo ambalo Malindi ilishinda kwa bao 2-0.

Katika mchezo huo mtafaruku ulianza kujitokeza dakika za nyongeza baada ya mmoja wa washambuliaji wa Kisiwani kufanya kosa eneo la hatari na kulazimika kupigwa penalti jambo lililowakasirisha washambuliaji wa timu hiyo na kuanza kufanya vurugu uwanjani hadi kushindikana kupigwa penalti hiyo.

Washambuliaji hao walianza kumpa kichapo mwamuzi msaidizi namba moja Abdalla Said na wengine wakiwakimbiza mbio hadi nje ya uwanja kwa lengo la kutaka kuwaadhibu wakidaiwa kushindwa kuzitafsiri vyema sheria 17 za Soka.

Vilevile, viongozi wa Kisiwani walianza kutoa maneno makali wakidai waamuzi wanawaonea huku wakisahau kuwa wanatoka mbali na gharama kubwa wanazotumia kufika uwanjani.

Mashabiki wa soka visiwani hapa akiwemo Suleiman Said na Habib Ali wameuomba uongozi wa Shirikisho la Soka Zanziba - Kanda ya Pemba kuhakikisha wanasimamia kikamilifu michezo hiyo ili kuepusha matatizo yasiyo ya lazima uwanjani yasijitokeze.

Walisema ni lazima shirikisho hilo lichukue hatua za kisheria kama mchezaji au mwamuzi atakabainika kuhatarisha amani uwanjani kwani matendo hayo yanaweza kuchafua soka visiwani Zanzibar.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz