Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahuni ni wahuni tu, hawana muda wala hawajali

Gsm Hersi Arafati (22).jpeg Wahuni ni wahuni tu, hawana muda wala hawajali

Thu, 23 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahuni wa mjini walimuuza Fiston Mayele tena straika wa hatari kabisa ila leo hii Wahuni wanachekea chooni kuwa Stephen Aziz Ki amefikisha mabao 17 ambayo Mayele alifikisha msimu uliopita na hapo bado Aziz Ki ana mechi mbili mkononi, Wahuni sana hawa.

Wahuni hawa wanamruhusu Joyce Lomalisa Mutambala aondoke Jangwani wakati ambao yupo kwenye kiwango bora kabisa, wanajiamini tu na wameamua tu na tayari wana mbadala wake kutoka hapo Congo DR, Wahuni tu wanafanya mambo yao kihuni huni tu.

Wahuni wanataka kurudia walichokifanya msimu uliyopita, wanaweka na kuvunja rekodi, wanavunja na kuziweka na Wahuni ni kama hawana muda na hawajali sana! Wenetu wanabet sana hawana muda wanasikilizia mkeka utiki, washabetia ada na hawana muda.

Mwanzo mwa hii safari Mhuni mmoja anatokea Kinondoni na swahiba wake mkubwa ni Mkeyenge. Just imagine mwanetu Mkeyenge! Mhuni mwingine anatokea Unguja na Mwanae mkubwa anauza juice ya ukwaju pale Michenzani, just Imagine! Wahuni ni wahuni tu!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live