Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagosi wa Kaya ni mvinyo ghali kutoka Tanga

Bao Full Wagosi Wagosi wa Kaya ni mvinyo ghali kutoka Tanga

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umepata kuusikia mvinyo wa Domaine de la Romanee – Conti? Ni 1945 vintage. Bei mbaya zaidi duniani. Chupa moja inauzwa dola 558,000 (Sh1.4 bilioni).

Wanasema thamani ya mvinyo ni umri wake. Miaka inavyoongezeka na ubora huongezeka. Kwa ukweli huo, basi ndivyo kwa Wagosi wa Kaya. The Bongo Flava 2001 vintage, lakini 2023, wamekuwa watamu asali inaomba poo!

Jana (Oktoba 27, 2023), ilikuwa siku ya Wagosi kutabaruku jukwaa la Alliance Francaise, Upanga. Ni shughuli ya Bongo Flava Honors, kuthamini mchango wa Wagosi kwenye ujenzi na ukuaji wa Bongo Flava.

Kilichotokea, Wagosi walishusha ladha kipeo cha pili. Haikuwa ngano ya ng’ombe hazeeki maini, ulikuwa udhihirisho kuwa zile mtu bee; Genius Mkoloni na Dr John, zililetwa duniani kufanya mwafaka na mic.

Kigoma cha Mdumange ndio kilianzisha shoo. Mkoloni na Dr John wanaonesha umahiri wa kupiga ngoma na kuimba nyimbo asilia ya Tanga. Kisha, ngoma pembeni, wimbo “Bao” unasababisha audience iumie mbavu kwa vicheko.

Ah ha-a-ha-a-ha-a kapwi-ii, “Taxi Driver” ipo kwa hewa. Wagosi wanatoa kifurushi chenye huduma tatu; muziki, futuhi na ujumbe wa maisha ya kila siku.

Energy ya Wagosi ni super-voltage. Sauti zao zina nguvu ajabu. Miili yao ina nishati kupitiliza. Ufanisi wao kwenye “Kibaka Kaokoka”, ndio uleule kwenye “Traffic”, “Tanga Kunani” hadi “Wauguzi”.

Kuna walioona ni performance bora ya muziki. Wengine walitafsiri ni burudani kamili ya sanaa. Mimi niliona entertainment masterclass. Wagosi walipiga shoo, huku wakiwaingiza watu darasani jinsi burudani inavyopaswa kutolewa.

It was a well spent night, maana kabla ya Wagosi, Sugu The Jongwe alishusha bando heavy with Big Dog Pose. Wimbo “Muda Mrefu” unaamsha balaa. Sugu with PDP, ile moment ni mchoro wa indelible marker. Haufutiki!

Wale Swahili Blues Band ni magnificent. Wanaunda ala za nyimbo na kuzinogesha, muziki unakuja masikioni ukiwa super. Dani Msimamo naye super. Alifanya poa sana with Wagosi.

Halafu kuna tofauti kubwa kati ya DJ set na set za Boniluv. Aisee, Boni naye ni mvinyo expensive. Umri unavyokwenda ndivyo anazidi kuwa mbaya kwenye mashine.

You gotta love Bongo Flava Honors

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live