Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wageni walitumwa kutikisa nyavu VPL

WAGENI+PIC Wageni walitumwa kutikisa nyavu VPL

Mon, 27 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By THOMAS NG'ITUMASTRAIKA wa kigeni wa Simba, Azam na Yanga, Meddie Kagere, Obrey Chirwa na David Molinga ndiyo waliofunika kwa upachikaji wa mabao katika msimu wa Ligi Kuu Bara uliomalizika jana Jumapili.

Pamoja na kwamba Kagere ameshindwa kuifikia rekodi yake ya mwaka juzi alipofunga mabao 23 msimu uliopita amefunga mabao 22 lakini ameisaidia timu yake ya Simba kutwaa taji la ligi kwa miaka mitatu mfululizo ikimaliza na pointi 88.

Chirwa anayekipiga Azam amefunga mabao 12 lakini timu yake imeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 70. Yanga na Azam sasa wanaomba dua ili Tanzania ipate uwakilishi wa timu nne kwenye michuano ya kimataifa ya Afrika.

Molinga raia wa Congo anayeichezea Yanga, amefunga mabao 11 licha ya kutoanza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ambapo amechangia kwa kiasi kikubwa kuisaidia timu yake kumaliza msimu huo ikiwa na pointi 72.

Yanga imeshika nafasi hiyo baada ya kuifunga Lipuli bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi uliochezwa Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Nyota wa Namungo, Blaise Bigirimana raia wa Burundi amefunga mabao 11 sawa na Molinga ambapo ameisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne msimu wa ligi uliopita.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz