Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wageni wa Ligi kufungua msimu leo

Cda Wageni Ligi Wageni wa Ligi kufungua msimu leo

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo tutapata fursa ya kushuhudia timu mbili ngeni kwenye Ligi ya NBC 2023|24 [Mashujaa FC na Tabora United] zikicheza mechi zao za kwanza.

TABORA UNITED imepanda Ligi Kuu ikijulikana kama Kitayosce FC, imesajili wachezaji wengi wa kigeni ambao pia ni wageni kwenye Ligi sio wa kuchukua Simba, Yanga au Azam FC.

Imemchukua Kocha wa zamani wa Simba Goran Kopunovic ambaye aliwapa nafasi vijana wengi wa Simba kama Ibrahim Ajib na Said Hamis Ndemla. Kwa hiyo Tabora United haijaja Ligi Kuu kinyonge.

MASHUJAA FC ni timu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ] wachezaji wake wote ni raia wa Tanzania, ipo chini ya Kocha mpya Abdallah Barres.

Leo Mashujaa FC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar ambayo ni timu kongwe kwenye Ligi ya Kuu ya Tanzania.

TABORA UNITED na MASHUJAA FC ni timu ngeni kabisa kwenye Ligi, zitaweza kubaki kwenye Ligi? Hilo ndio swali ambalo wadau wengi wanajiuliza!

RATIBA LIGI KUU YA NBC

MASHUJAA FC V/s KAGERA SUGAR Lake Tanganyika Stadium, Kigoma Saa 10:00 jioni

AZAM FC V/s KITAYOSCE Azam Complex, Chamazi, Dar Saa 1:00 usiku

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: