Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waganga wa Peru wakomaa na Neymar mchana kweupe

WhatsApp Image 2023 09 13 At 09.jpeg Waganga wa Peru wakomaa na Neymar mchana kweupe

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la waganga wa kienyeji kutoka msituni, milimani na pwani za Taifa la Peru ambao hufahamika kama Tayta Inti (Father Sun) waungana kumzuia winga wa Timu ya Taifa Ya Brazil, Neymar, kuelekea mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Waganga hao walitambika nje ya uwanja wa taifa wa Peru huku kukiwa na sanamu iliyomuwakilisha Neymar ikiwa imefungwa, pia wakiwa na mapanga, hirizi, bendera na picha za wachezaji wa timu zote mbili.



Mganga aliyefahamika kwa jina la Shaman Felix Rondan aliwaambia waandishi wa habari kuwa,

“Tunampunguza makali Neymar kwa kumfunga miguu. Tumemfunga ili asiwe katika hali nzuri, asicheze vizuri.”



Timu ya Taifa ya Peru inahitaji alama baada kutoka sare dhidi Paraguay, huku Brazil wakishinda mchezo wao wa ufunguzi kwa bao 5-1 dhidi ya Bolivia, ambapo Neymar alipachika mabao mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live