Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanya kazi Man United wabanwa walalama

Man United Wafanyakazi Wafanya kazi Man United wabanwa walalama

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabosi wa Manchester United wameondoa utaratibu wa kugawa chakula cha mchana kwa wafanyakazi wanaokuwepo siku ya mechi na kupunguza idadi ya vitu walivyokuwa wanawafanyia mashabiki maalum ikiwa ni mwendelezo wa kupunguza gharama za matumizi.

Sir Jim Ratcliffe na timu yake ya INEOS walianza kwa kuhakikisha wanabana bajeti mara tu baada ya kununua hisa za asilimia 25 mapema mwaka huu na walipunguza karibia wafanyakazi 250.

Sasa wamehamia katika mambo mengine ambayo wanaamini yanaweza kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji timu.

Awali wafanyakazi wa uwanja ikiwemo walinzi na maofisa wengine walikuwa wakipewa chakula na viwanyaji walipokuwa wanafanyakazi siku ya mechi lakini utaratibu huo umeondolewa na haukuwepo kabisa katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Fulham wiki iliyopita.

Baadhi waliambiwa wanaweza kula chakula kilichoachwa na baadhi ya maofisa wa kampuni zinazoidhamini Man United baada ya kuwa kingi.

Ripoti zinaeleza moja ya sababu zilizofanya viongozi wa mashetani hao wekundu wasitishe mpango huo ni vyakula vingi vilikuwa vikibakishwa na kwenda kutupwa jambo ambalo ni hasara.

Baadhi ya wafanyakazi pia wamedai wanalazimishwa kula chooni: “Wameweka meza ya kulia chakula karibu na vyumba vinne vya choo,” akasema mmoja. “Unatoka chooni unakuta mtu ameketi mbele yako, akila.”

Hata hivyo, Man United imepinga hilo ikisisitiza wametenga chumba maalum cha kulia chakula lakini baadhi ya wafanyakazi wanachagua kula katika eneo hilo la karibu na choo kwa sababu ya utulivu wake.

Kabla ya mchezo kuanza mashabiki walikuwa wakipewa vipeperushi na jarida la kusoma wakati mchezo unaendelea, utaratibu huo pia umeharibiwa ikielezwa nusu tu ya mashabiki ndio walipata huku Man United ikisema wamefanya hivyo kwa sababu majarida mengi yamekuwa yakitupwa baada ya mechi jambo linaloashiria mashabiki wengi hawasomi.

Vitu vingi vilivyokuwa vinapatikana hapo awali kwa sasa vimeondolewa ikiwa na baadhi ya wafanyakazi walishangazwa na kilichotokea msimu uliopita walipoambiwa wajigharimikie nauli za kwenda katika fainali ya FA dhidi ya Man City jambo ambalo zamani lilikuwa ni chini ya timu.

Marupurupu mengine kwa wafanyakazi wenye vyeo vikubwa, kama vile tafrija ya kabla ya mechi, chakula cha mchana baada ya mechi na malazi ya hoteli, yaliondolewa kabisa.

Vilevile utaratibu wa wakurugenzi hao kuleta marafiki na familia zao kwenye mechi kubwa za Wembley uliondolewa na walitakiwa walipie.

Chanzo: Mwanaspoti