Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu kiundani wapinzani wa Simba Sc (US Gendarmerie)

Usgn Niger S.jpeg Kikosi cha USGN

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANAITWA Union Sportive de la Gendarmerie Nationale (Us Gendermerie) ni timu kutoka Niger, inapatikana Niamey mji mkuu wa Niger...timu ilianzishwa mwaka 1996, miaka 26 nyuma.

US Gendermerie wanamiliki uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000, ujulikanao kama Stade Général Seyni Kountché. Ndio mabingwa wa Niger Premier League na Niger Cup, msimu uliopita.

US Gendermerie msimu uliopita kwenye mashindano ya Caf Confideration Cup walitolewa kwenye hatua ya kwanza (First Round). Na msimu huu kwenye Caf Champion League walitolewa na Al Ahly kwenye mchezo wa Kwanza walitoka sare ya (1-1) uko Niger na mchezo wa pili wakipoteza kwa kipigo kikubwa cha magoli (6-1) Misri.

Wanao wachezaji hatari kama B. Hainikoye anaecheza kiungo mshambuliaji na mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi chao V. Adebayor pia ni kiungo mshambuliaji mwenye magoli mawili mpaka sasa.

Mwenendo wa Matokeo wakiwa uwanja wao wa Nyumbani.

USGN 2-0 Motema Pembe USGN 1-1 Al Ahly USGN 1-1 Le Messeger Ngozi USGN 1-2 Kabylie USGN 1-1 Yeelen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live