Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu Power Dynamos wapinzani wa Simba SC CAFCL

Dynamoooos Wafahamu Power Dynamos wapinzani wa Simba SC CAFCL

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Power Dynamos ni klabu ya Mpira wa Miguu ya Zambia yenye Makao Makuu yake mjini Kitwe ambayo inacheza katika kitengo cha MTN/FAZ Super Division.

Uwanja wao nyumbani wa Power Dynamos ni Urthur davies Stadium uliopo mjini Kitwe ukiwa na uwezo wa kubeba Mashabiki 12, 000, Power Dynamos kwa sasa inafadhiliwa na Copperbelt Energy Corporation.

Power Dynamos iliyoanzishwa mwaka 1971 inajulikana kwa kucheza soka maridadi la pasi, na mechi zao kwa kawaida hufurahiwa na mashabiki wa Ligi Kuu ya Zambia.

Wapinzani wao wakuu ni Nkana FC na Zesco United FC, Michezo inayohusisha Power Dynamos na klabu yoyote kati ya hizi mbili huwa inahudhuriwa na mashabiki wengi wa soka nchini humo.

Mnamo 1991, klabu ya Power Dynamos ilikuwa klabu ya kwanza kusini mwa Afrika kushinda taji la Bara baada ya kushinda Kombe la Washindi wa Kombe la Afrika.

Power Dynamos ndio Mabingwa wa msimu uliomalizika 2022/2023 na Watashiriki CAF Champions League msimu ujao wa 2023/24.

Performance in CAF competitions CAF Champions League: 3 appearances 1998 – Second Round 2001 – First Round 2012 – Second Round African Cup of Champions Clubs: 2 appearances 1985 – Second Round 1995 – First Round

CAF Cup Winners’ Cup: 10 appearances 1981 – Quarter-finals 1982 – Finalist 1986 – Quarter-finals 1988 – Second Round 1989 – Second Round 1991 – Champion 1992 – Second Round 1994 – First Round 1999 – Quarter-finals 2003 – Quarter-finals.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live