Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu Club Africain wapinzani wa Yanga Shirikisho

Club Africain Yanga Wafahamu Club Africain wapinzani wa Yanga Shirikisho

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Club Africain ni miongoni mwa klabu chache kongwe Barani Afrika, ilianzishwa miaka 102 iliyopita (mwaka 1920), ikijulikana kwa jina maarufu “El Club” kabla ya kubadilishwa jina.   Klabu Africain ndio timu ya pili kwa ukubwa na ya pili kwa mafanikio makubwa nyuma ya klabu ya Eparance Sportive de Tunis iliyoanzishwa mwaka 1919 huko nchini Tunisia.

Club Africain ndio Klabu ya kwanza kutoka Tunisia kushinda “International Trophy” ambapo walishinda Maghreb Cup Winners mwaka 1971.

Baada ya miak 20 (yaani mwaka 1991) Club Africain ikawa klabu ya kwanza kutoka Tunisia kushinda CAFCL kwa kipindi hicho iliitwa African Champions League.

Katika mafanikio ya ligi ya ndani inashika nafasi ya pili ikiwa ina jumla ya mataji rasmi 39 nyuma ya Esparence wakiwa na mataji rasmi 53.

Kwenye ligi kuu ya nchini Tunisia Club Africain ametwaa jumla ya mataji 13 akishika nafasi ya pili nyuma ya Esparence wenye jumla ya mataji 32 akiwa ndiye kinara wa mataji katika ligi hiyo.

Kwenye mafanikio ya kimataifa Club Africains wamewahi kuwa mabingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika katika msimu wa mwaka 1991 akimfunga SC Villa ya nchini Uganda kwa jumla ya mabao 7-2 mechi zilichezwa mbili nyumbani na ugenini,ugenini ilikuwa sare 1-1 na nyumbani Cluba Africains walishinda 6-1.

Kwenye historia ya kombe la Shirikisho hawajawahi kubeba ubingwa wa michuano hiyo lakini waliwahi kufika fainali mwaka 2011 na kufungwa kwa penati 6-5 na klabu ya Maghreb Association Sportive de Fès ya nchini Morocco.

Licha ya historia kubwa ya timu hiyo,wamekuwa na rekodi mbaya kwani wameshindwa kubeba kombe lolote tangu msimu wa mwaka 2018 walipobeba ubingwa wa kombe la Tunisia (sio ligi kuu).

Mara ya mwisho kubeba ubingwa wa ligi kuu ilikuwa katika msimu wa mwaka 2015 na kuanzia hapo hawajawahi kumaliza hata katika nafasi ya pili katika ligi hiyo,yote hayo yanatokana na anguko kubwa la kiuchumi ndani ya timu hiyo.

Msimu uliopita walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 4.

Club Africain wanatumia Uwanja wa Stade Olympique De Rades unaochukuwa watazamaji 60,000 kama ulivyo Uwanja wa Taifa.

Club Africain imefanikiwa kutwaa makombe 13 ya ligi ya Tunisia na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2015, huku kombe la Tunisia Cup wakitwa mara 13.

Mara ya mwisho wakimfunga Ètoile de Sahel kwa magoli 4-1 mwaka 2018 na makombe matatu ya Tunisia Super Cup.

Larry Azounl ndio anatajwa kuwa mchezaji hatari kwenye kikosi hicho akiwa amesajiliwa €600,000 (zaidi ya Tsh bilioni 1.37) mwaka 2021 akiwa na miaka 28. Larry alishawahi kuchezea timu ya vijana ya Ufaransa.

Kwenye hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Club Africain ilianzia hatua ya pili ya mtoano ambapo walicheza na Kipanga FC ya Zanzibar, mechi ya kwanza Kipanga wakiwa nyumbani walitoa sare ya bao 0-0.

Mechi ya marudiano Kipanga walikubali kupokea kipigo cha bao 7-0 na kuondoshwa katika michuano hiyo kwa aggregate ya magoli 7-0.

Kigingi kingine kwa Wananchi! Ni muda wa Yanga kuonesha ukubwa wao kwenye Mashindano ya Kimataifa.

Club Africain wamepangwa kukutana na Yanga katika Playoffs ya michuano ya kombe la Shirikisho na wataanzia ugenini taifa Novemba 2 na kumalizia nyumbani kwao Tunisia Novemba 9, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live