Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu Al Ahli Tripoli wapinzani wa Simba SC CAFCC

Al Ahli Tripoli Sa Al Ahli Tripoli

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi Klabu ya Simba imethibitisha kuwa itakutana na Klabu ya Al Ahli Tripoli ya nchini Libya.

Klabu ya Simba itaanzia ugenini katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Kombe la Shirikisho 24/25.

Al Ahli Tripoli ilishinda michezo yake yote miwili Dhidi ya Uhamiaji FC ya Zanzibar.

Uhamiaji FC 0-2 Al Ahli Tripoli

Al Ahly Tripoli 3-1 Uhamiaji FC

Al Ahly Tripoli imepita kwa Aggregate 5-1

Michezo ya Simba Dhidi ya Al Ahli Tripoli.

Al Ahli Tripoli Vs Simba

13-15 Septemba 2024

Simba Vs Al Al Ahli Tripoli

20-22 Septemba 2024

Al Ahli Tripoli imejiongezea kikosi kuelekea msimu mpya kwa kufanya sajili maeneo mbalimbali.

▪️Majina kamili; Wanaitwa Al Ahli Tripoli Sports Club kutoka nchini Libya na wanafahamika pia kwa jina la utani la Bianco Verde (Timu ya Karne)

▪️Timu hii ilianzishwa Septemba 19 1950, Klabu namba mbili yenye mafanikio zaidi katika soka la Nchi ya Libya

▪️Wamepata nafasi ya kucheza Kombe la shirikisho msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Al Nassr na Al Hilal za Libya.

➜ Wanatumia uwanja wa Tripoli stadium kwenye michuano ya CAF. Rangi rasmi za Al-Ahli Tripoli ni Kijani. Ubingwa wao wa kwanza wa ligi kuu walitwaa mwaka 1964.

➜ Msimu uliopita 23|24 walikuwa vinara wa kundi (B) katika ligi kuu ya Libya ambayo huchezwa kwa makundi mawili.

◉ 20 - Michezo.

◉ 15 - Michezo waliyoshinda.

◉ 03 - Sare | Suluhu.

◎ 02 - Kupoteza.

Baada ya hapo ligi hiyo hukutanisha timu zilizofanya vizuri katika kila kundi kupata Bingwa ambapo Al-Ahli Tripoli walishika nafasi ya (3) na kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya CAF Confederations cup.

➜ Katika dirisha kubwa lililopita wamesajili wachezaji wafuatao kwenye kikosi chao :

◉ Mabululu (CF) ›› Al-Ittihad ????????

◉ Hamdou El Houni (W) ›› Wydad ????????

◉ Al Gozoli (CMD) ›› Free agent.

◉ Soufian Bendao (CB) ››

◉ Tarek Bshara (W) ››

Mafanikio yao makubwa :

Ubingwa wa ligi kuu ×13

1964, 1971, 1973, 1974, 1978, 1984, 1993, 1994, 1995, 2000, 2014, 2016, 2023.

Ubingwa wa (FA) ×7

1976, 1994, 2000, 2000, 2006, 2016, 2023.

×2 Libyan Super Cups

Champions league appearances :

◉ 2000 - First round.

◉ 2009 - Second round.

◉ 2015 - Preliminary round

◉ 2016 - Second round

◉ 2017 - Quarter final.

Confederations cup appearances:

◉ 2007 - Preliminary round.

◉ 2009 - First round.

◉ 2010 - First round.

◉ 2014 - Preliminary round.

◉ 2016 - Group stage.

◉ 2022 - Semi final.

CAF cup winners:

◉ 1984 - Fainali ›› Withdrew

◉ 2002 - Second round.

▪️MAFANIKIO YAO MAKUBWA ZAIDI AFRIKA

Al Ahli Tripoli wamecheza Robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mara moja & Mwaka 2022 walicheza Nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika wakatolewa na Orlando Pirates ambao walimuondoa Simba SC kwa Matuta

1st Leg | Al Ahli Tripoli 0-2 Orlando Pirates

2nd Leg| Orlando Pirates 0-1 Al Ahli Tripoli

▪️Wwachezaji ghali zaidi: Staa wa Angola, Straika wa Magoli Agustinō Cristovao Pacienćia "MABULULU"???????? (32) ndiye mchezaji Ghali zaidi katika kikosi hicho akisajiliwa katika dirisha hili kwa Bil 2 za Kitanzania

Mchezaji mwingine ghali zaidi katika Kikosi chao ni Winga Hamdoi El Houni???????? (30) aliesajiliwa kutoka Wydad Casablanca kwa uhamisho wa bure ana thamani ya Mil 800+ za Kitanzania

▪️Kocha Mkuu: Kocha mkuu wa Klabu hii ni Chokri Khatoi raia wa Tunisia???????? ambae amewahi kupita Abu Salim ya Libya na Stade Tunisien ya Tunisia

▪️Top Scorer: Ahmed Mohammed Rajab Krawas (35) ndiye nyota aliefunga mabao mengi zaidi katika msimu uliomalizika (12)

▪️Al Ahli Tripoli wanatumia Uwanja wa Libya Tripoli International kama uwanja wao wa nyumbani wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 45,000 waliokaa

Wanatumia jezi za kijani katika mechi zao za nyumbani na wanatumia rangi Nyeupe wakiwa Ugenini

▪️Thamani yao: Kwa mujibu wa Transfer Market thamani ya Kikosi cha Al Ahli Tripoli ni Bil 6 za Kitanzania.

▪️Mara ya mwisho kwa Al Ahli Tripoli kucheza katika Ardhi ya Tanzania ilikua ni mwaka 2021 wakipoteza 2-0 kwa Biashara United Mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live