Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadudu wasumbua Euro 2024

Wadudu EURO Wadudu wasumbua Euro 2024

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

KAMBI ya mastaa wa Ujerumani kwenye fainali za Euro 2024 imekuwa ya moto kwa wachezaji baada ya mbu kuvamia na kusumbua kuliko kawaida.

Kikosi hicho cha Kocha Julian Nagelsmann kimewapa burudani mashabiki wake baada ya kutinga hatua ya 16 bora, lakini wachezaji wenyewe wanakutana na balaa zito huko kwenye kambi yao kutokana na shambulio la mbu.

Kipa veterani wa kikosi hicho, Manuel Neuer alisema wanalazimika kukaa kwenye vyandarua ili kujikinga na maumivu ya kung’atwa na mbu.

Staa huyo wa Bayern Munich, Neuer, 38, alisema: “Tunahitaji kuhakikisha vyandarua vya mbu vinashushwa kila muda tunaokuwa tunatazama mechi kwenye televisheni zilizopo kwenye bwawa la kuogelea.”

Kocha Nagelsmann alisema: “Tumevamiwa na mbu wasiokuwa wa kawaida. Tunahitaji kupambana na huu upepo unaoleta mbu kwa sababu kwenye eneo hili awamu hawaku wengi. Na kama hali itakuwa mbaya zaidi, tutahamia ndani ofisini.”

Straika Maximilian Beier, 21, aliongeza: “Nimeshang’atwa na mbu mara mbili au tatu.

“Lakini, kama ni mbu tu ndiyo tatizo letu kubwa tulilonalo, basi hilo halina shida.”

Kutokea kwa mafurukio kusini mwa Ujerumanina kuwapo kwa kipindi hiki cha majira ya joto kumechangia kuongezeka kwa wadudu hao.

Mtaalamu wa masuala ya wadudu, Martin Geier alisema: “Mbu wanasuambulia sana, wamekuwa kwenye makundi makubwa, wanang’ata kwelikweli nyakati za mchana na usiku pia.”

Hii si mara ya kwanza kwa kikosi hicho cha Ujerumani kuandamwa na wadudu kwenye fainali hizo za Euro 2024 zinazofanyika kwenye ardhi ya kwao, baada ya nyuki kuvamia Stuttgart Arena siku ya kuamkia mchezo wao dhidi ya Hungary wiki iliyopita.

Zimamoto walilazimika kuvaa mavazi maalumu ya kujikinga na nyuki na kwenda kuwaondoa baada ya kujenga kiota kwenye bango la biashara lililopo pembezoni mwa uwanja huo.

Ujerumani iliyopangwa Kundi A katika fainali hizo za Euro 2024 sambamba na timu za Uswisi, Hungary na Scotland imemaliza kinara kwenye kundi hilo baada ya kukusanya pointi saba katika mechi tatu, ikishinda mbili na kutoka sare moja, huku ikiwa imefunga mabao manane na kuruhusu mawili tu kwenye nyavu zao.

Kwenye orodha hiyo ya mabao manane iliyofunga, moja lilikuwa la staa wa Scotland kujifunga, huku wakali wa kikosi hicho waliofunga ni Niclas Fulkrug na Jamal Musiala mara mbili kila mmoja, huku mastaa wengine waliofunga mara moja moja ni Emre Can, Ilkay Gundogan na Kai Havertz.

Chanzo: Mwanaspoti