Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wafurika hafla kuzichangia timu za Taifa

Hafla Johari Rotana Wadau wafurika hafla kuzichangia timu za taifa

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Idadi kubwa ya wadau wa michezo imejitokeza katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam kushiriki hafla ya kuzichangia timu za taifa inayofanyika leo.

Hafla hiyo inaongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambapo fedha zitakazopatikana zitagawanywa kwa timu za taifa za michezo mbalimbali.

Miongoni mwa wadau wakubwa wa michezo ambao wamejitokeza kwenye hafla hii ni Waziri wa Fedha, Mwigullu Nchemba ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Yanga.

Ukiondoa Mwigullu kuna kundi kubwa la wafanyabiashara na viongozi wa vyama tofauti vya michezo ambao wanashiriki harambee hii.

Wapo pia watumishi wa wizara ya sanaa, utamaduni na michezo akiwemo kaimu mkurugenzi wa michezo Tanzania, Ally Mayay.

Kuna uwepo pia wa wachezaji wa zamani wa soka na michezo mingine mmojawapo akiwa ni nyota wa zamani wa Taifa Stars, Adolph Rishard.

Hafla hii inafanyika ikiwa ni siku chache kabla ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuanza kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) huko Ivory Coast ambazo zitaanza Januari 13 hadi Februari 11.

Katika fainali hizo za AFCON mwaka huu Tanzania imepangwa katika kundi F na timu za Morocco, Zambia na DR Congo.

Januari 17 Tanzania itacheza na Morocco, mechi ya pili itakuwa Januari 21 dhidi ya Zambia na itamaliza kwa kuikabili DR Congo, Januari 24.

Chanzo: Mwanaspoti