Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wacongo wamlilia Maxi Nzengeli

Maxi Nzengeli X Congo Winga mpya wa Yanga Maxi Nzengeli

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya AS Maniena imeeleza masikitiko yake kuondokewa na Winga wao mahiri Maxi Mpia Nzengeli aliejiunga na Klabu ya Yanga na juzi jumamosi alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa Yanga.

Akizungumza CEO wa klab ya As Maniema ya Congo DR, Esther Kumba amesema;

“ Inapotokea ndani ya klab yako ukaondokewa na Mchezaji Muhimu basi lazima kwanza utulie, Utulize akili ilinuoate mtu sahihi wa kuvaa viatu vyake, Nikweli Max alikuwa Mhimili Mkubwa sana ndani ya klab yetu na hakuwa tu mchezaji bali alikuwa kiongozi zaidi ya Mwalimu pale timu ilipohitaji Matokeo pale inapokosa matokeo, ”

“ Kwasasa tumekamilisha usajili wa Japhe Kitambala akitokea To Mazembe ili aje avae viatu vya Max Nzengeli alihejiunga na Mabingwa wa Tanzania Young Africans, ”

Tayari Maxi Nzengeli ameshaanza kukonga mioyo ya Wanayanga kwa soka aliloonesha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs.

Je ni kweli wana haki ya kumlilia Maxi Nzengeli?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live