Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wote 12 waliosajiliwa Simba ni magarasa?

Simba Sc Usajili Wachezaji wote 12 waliosajiliwa Simba ni magarasa?

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wote 12 ambao Klabu ya Simba imewasajili msimu huu, hakuna hata mchezaji mmoja ambaye angalau timu yake aliyokuwa akiitumikia imemaliza nafasi mbili za juu kwenye msimu wa Ligi ya nchi aliyokuwa anaichezea.

Kitakwimu inaonesha, timu walizokuwa wakicheza nyota hao wameshindwa kuzisaidia angalau kucheza mashindano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

Wachezaji waliosajiliwa na Simba msimu huu ni kama ifuatavyo;

1. Steven Mukwala katoka Asante Kotoko ambayo ipo nafasi ya 6 Ligi Kuu ya Ghana

2. Augustine Okejepha katoka Rivers ambayo ipo nafasi ya 8 Ligi Kuu Nigeria

3. Debora Fernandes Mavambo katoka Mutondo ambayo ipo nafasi ya 13 Ligi Kuu Zambia

4. Joshua Mutale katoka Power Dynamos ambayo ipo nafasi ya 3 Ligi Kuu Zambia

5. Valentino Mashaka katoka Geita Golfd FC iliyoshuka daraja Ligi Kuu Tanzania Bara

6. Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka SuperSport United FC ambayo ipo nafasi ya 7 Ligi Kuu Afrika Kusini

7. Omary Abdallah Omary kutoka Mshaujaa FC ambayo ipo nafasi ya 8 Ligi Kuu Tanzania Bara

8. Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ambayo ipo nafasi ya 6 Kundi A, Ligi Kuu ya DR Congo (Ligi ya Congo ina Makundi mawili, A na B)

9. Karaboue Chamou kutoka Racing Club d' Abidjan ambayo iko nafasi ya 3 Ligi Kuu ya Ivory Coast

10. Yusuph Kagoma Singida kutoka Big Stars ambayo ipo nafasi ya 11 Ligi Kuu Tanzania Bara

11. Ahoua Jean Charles katoka Stella Club d'Adjamé ambayo ipo nafasi ya 5 Ligi kuu ya Ivory Coast

12. Lameck Lawi kutoka Coastal Union ambayo ipo nafasi ya 4 Ligi Kuu Tanzania Bara (usajili wake bado una sintofahamu).

Swali ni je, wataweza kuisaidia Simba SC ambayo imemaliza ligi katika nafasi ya tatu, kupata ubingwa wa Ligi mbele ya Yanga SC na Azam FC ambao wamejidhatiti msimu ujao kufanya vizuri zaidi.

Msimamo wa Ligi ni kigezo kidogo sana cha kutoa majibu ya ubora wa mchezaji, bali ubora wa mchezaji unajengwa nay eye mwenyewe, wachezaji wanaomzunguka, benchi la ufundi, vifaa vya mazoezi, nafasi ya kucheza na ubora wa kikosi ambacho atakuwepo sambamba na mashindano husika, hivyo nyota hao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa Simba mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live