Ikiwa ni mchezo kati ya Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, dhidi CR Belouizdad, mehci ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopewa jina maalumu la 'Pacome Day', huku mashabiki na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakipaka rangi vichwa vyao, nyota wazawa ni kama wameigomea kimtindo 'blichi'.
Uongozi wa Yanga uliipa jina hilo kama Pacome Day ikihamasisha wadau wajiweka kana nyota wa timu hiyo anayeoongoza kwa mabao kwa klabu hiyo katika michuano hiyo, Pacome Zouzoau na wadau kibao wameweka nywele zao blinchi kumuunga mkono, lakini wachezaji wazawa wameonekana kutokubadili rangi za nywele zao kulinganisha na wenzao wa kigeni.
Wachezaji wa kigeni wa Yanga waliowasili uwanjani mapema kwa ajili ya pambano hilo la Kundi D, wamekuwa na muonekano tofauti unaoashiria kukubaliana na siku husika ya mwenzao Pacome, kiungo mwenye asili ya Ivory Coast ambaye muonekano wake wa siku zote ndio umekuwa alama katika siku hii muhimu kwa timu hiyo.
Ukiachana na viongozi na mashabiki kubadilisha mionekano yao na kufanana na mchezaji huyo lakini swali ni je kwanini wazawa wote hawajafanya mabadiliko hayo.
Wachezaji wa kigeni waliobadilisha nywele ni Stephane Aziz Ki, kipa Djigui Diarra, beki Yao Kouassi, kiungo mshambuliaji Augustine Okrah na straika Joseph Guede aliyeweka kwenye ndevu tu, huku mwenyewe Pacome naye akiwa hajabaki nyuma.
Idadi ya wachezaji hao ni karibu nusu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha mechi ambao kocha Miguel Gamondi hupenda kuwatumia kwenye mechi mbalimbali, lakini wazawa wakiichukulia poa hamasa hiyo.
Mwanaspoti halikufanikiwa kuzungumza na wachezaji wazawa ili kujua imekuwaje hawajabadili rangi za nywele zao ili kuunga mkono hamasa ya mchezo huo ulioshikilia matumaini ya Yanga kwenda robo fainali ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa, kwani tangu ilipobadilishwa kutoka Klabu Bingwa Afrika mwaka 1997 na kushiriki makundi ya mwaka 1998 haijawahi kufikia robo fainali tofauti na Simba iliyocheza mara tatu katika misimu mitano.
Hata hivyo, huenda kwa wazawa maadhimisho haya kwao yamekuwa si kipaumbele chao ukilinganisha na mechi husika ndio maana wamebaki kama walivyokuwa hapo awali, japo beki Dickson Job yeye kaupisha mshari kichwani we blichi kuonyesha kusapoti mtoko huo. Ibrajim Bacca na Metacha Mnata ni baadhi ya wachezaji ambao hawapata rangi hiyo.
Kikosi hicho kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Saa1:00 jioni kutafuta pointi tatu dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria ikiwa ni mchezo wa kufuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, timu zote zikiwa na pointi tano nyuma ya vinara na watetezi wa taji hilo, Al Ahly ya Misri yenye tisa baada ya jana usiku kuinyoa Medeama ya Ghana.
Yanga wameshinda mchezo huo kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na Mudathir Yahya, Stephane Aziz Ki, Kennedy Musonda na Joseph Guede na kuwafanya kuandika historia kwa mara ya kwanza kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.