Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wamvuruga Benchikha, abaki uwanjani peke yake baada ya sare

Benckhik0007 Abdelhak Benchikha

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba Benchikha jana amekaa benchi uwanjani zaidi ya dakika 20 baada ya mchezo dhidi ya Ihefu akiwaza kwa kina jambo la kufanya baada ya timu yake kukosa ushindi katika michezo minne mfululizo huku ikifungwa mechi tatu na kusare moja.

Tukio hilo lilitokea jana Aprili 13, 2024 baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa raundi ya 20 ya Ligi Kuu katika Dimba la CCM Liti mkoani Singida huku Simba ikiambulia sare ya bao 1-1.



Wakati wa mchezo, Benchikha alionekana kuchukizwa na kitendo cha mshambuliaji wake, Fred Michael kukosa bao la qazi jambo lililomfanya kocha huyo kukasirika, kuvua kofia yake na kuitupa chini kwa hasira.

Baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha aligoma kuambatana na kikosi chake kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambapo alisalia uwanjani kwenye benchi peke yake kwa muda kadhaa kabla ya kunyanyuka na kuondoka zake uwanjani hapo.

Ikumbukwe kuwa, Aprili 20, Simba atakuwa na kibarua kigumu mbele ya watani wao wa Jadi Yanga ambao wanaongoza Ligi wakiwa na alama 52 huku Simba akiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao 5-1 na Yanga kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live