Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji walishindwa kuchukua ubingwa misimu mitatu tunafyeka - Ahmed Ally

Inonga X Ngoma Wachezaji walishindwa kuchukua ubingwa misimu mitatu tunafyeka - Ahmed Ally

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amebainisha maeneo ambayo timu yao ilikosea na kusababisha kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano walioshiriki msimu huu ikiwemo Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB na Ligi ya Mabingwa Afrika huku akiongeza kuwa watayafanyia maboresho maeneo hayo kabla ya msimu mpya kuanza.

Ahmed amesema hayo jana baada ya Ligi Kuu kutamatika huku Simba wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambapo wameangukia kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ambayo watashiriki msimu ujao jambo ambalo amesema hayakuwa malengo yao kabisa.

“Kabla ya kuelekea kwenye Lifi na Kombe la Shirikisho msimu ujao lazima tufanye maandalizi marekebisho makubwa kwenye kikosi chetu. Timu tuliyo nayo lazima tuiboreshe kwa sababu hatuwezi kutoboa kwa namna tunavyoenda hivi sasa, lazima tulete watu wa kuja kutusaidia.

“Hili ndilo eneo tunaloenda kulifanyia kazi kwa asilimia kubwa zaidi. Unapofanya vibaya ujue kuna sababu nyingi na ukisema utatue sababu zote unaweza kusababisha tatizo jingine, hivyo tutaanza na hili kwanza la wachezaji, lazima tutafute wachezaji ambao watakuja kutimiza malengo yetu.

“Lazima ufanye tathmini kwa misimu mitatu tumekosa mataji, huyu mchezaji alikuwepo msimu wa kwanza nimekosa ubingwa, msimu wa pili alikuwepo nimekosa, msimu wa tatu alikuwepo na nimekosa ubingwa, nikienda naye msimu wan ne atanipa ubingwa? Tutafanya tathmini ya mchezaji mmoja mmoja kwa umakini ili tukifanya maamuzi yawe sahihi na bora kwa maslahi ya Simba,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live