Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji waliopewa nafasi jana Simba hawajaonesha kitu - Kiemba

Kiemba Wazawa Hawajaonesha Uwezo Wachezaji waliopewa nafasi jana Simba hawajaonesha kitu - Kiemba

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo Amri Kiemba amesema wachezaji wazawa wa Simba SC waliopewa nafasi jana hakuna kipya walichoonesha, wamefanya kawasaki sana.

Amesema mashindano ya Mapinduzi walimu huyatumia kuzoea kikosi lakini kwa wachezaji hao hawajamshawishi kitu mwalimu.

"Mashindano ya Mapinduzi ni sehemu ya mwalimu kuzoea kikosi chote hata wale ambao huwa hawapati nafasi.”

“Ukiangalia wale ambao wamecheza hauoni kama kuna kitu kipya, kwa mimi wameshindwa kunishawishi kwamba walikuwa wanastahili kwa zile kelele silizokuwa zinapigwa”

“Ushindi umepatikana jana kwa mchezaji mmoja mmoja hasa wale ambao walikuwa hawapati nafasi Chilunda, Duchu, Mwanuke ni kawaida sana kiasi kwamba ile level haitoshi kwa malengo ambayo Simba inayo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live