Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Wachezaji wajitahmini kwa kiwango kibovu"- Rooney

Skysports Graphic Manchester United 5559385 Wachezaji wa Man United wametakiwa kujitafakari

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amewataka wachezaji kujiuliza wao wenyewe kama wanatimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

Rooney amesema ni rahisi kumsukumia lawama mwalimu, kwa kuwa ndio muhusika wa kwanza.

Meneja wa Manchester, Ole Gunner Solskjaer anapitia kipindi kigumu kwa sasa na hasa baada ya kipigo cha magoli 5-0 kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita.

Matarajio yalikua makubwa kuelekea msimu huu kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kutumika katika kufanya usajili wa Ronaldo, J. Sancho lakini baada kupoteza michezo mitano ndani ya michezo takriban 10, kuna maswali yanaibuka kama aidha ulikuwa ni usajili sahihi.

"Kuna uwajibikaji mkubwa kwa wachezaji wao wenyewe, ni wachezaji wa viwango vya dunia, matokeo kwao ni muhimu " amesema Rooney

"wanatakiwa kuumia wanapopoteza mchezo hiyo itawafanya kuzingatia na kujituma mchezo ujao"

Manchester United itavaana na Tottenham mwishoni mwa wiki kule London, na inatazamiwa kuwa ni kimoja kati ya vipimo vya kuamua kumbakisha ama kumfukuza Ole Gunner Solskjaer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live