Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wa Ivory Coast wajazwa mamilioni na nyumba za kifahari

Ivory Coast ADaG1.jpeg Wachezaji wa Ivory Coast wajazwa mamilioni na nyumba za kifahari

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast wakifurahia ushindi katika fainali ya kombe la AFCON.

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae walizawaidia pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo Jumanne kusherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.

Tembo wa Ivory Coast waliishinda Nigeria katika fainali siku ya Jumapili na kunyakua taji hilo kwa mara ya tatu.

Kila mchezaji alipewa milioni 50 za sarafu ya CFA na nyumba ya kifafari yenye thamani sawa na pesa hizo.

Kocha Fae alipewa milioni 100 za sarafu ya CFA kwa kuongoza vizuri wachezaji wake baada ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu aliyetimliwa Jean Louis Gasset katikati ya mashindano kufuatia kipigo kibaya cha mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea.

“Mmeleta furaha kwa wanainchi wote wa Ivory Coast, hongera, hongera,” alisema Rais Alassane Ouattara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live