Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wa Azam FC ni kama hawajitambui - Kocha

Jamhuri Kiwhelu Julio Kocha Julio.

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha maarufu wa soka nchini, Jamhuri Kihwelo 'Julio', amesema moja ya sababu inayowakwamisha Azam FC ni kutojituma kwa wachezaji wanaosajiliwa katika klabu hiyo ambao mara nyingi wamekuwa wakiridhika na pesa nyingi wanazolipwa.

Julio amesema hayo mara baada ya Azam FC kufungashiwa virago kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika hivi karibuni kwa kuondolewa na Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia licha ya Azam kufanya usajili mkubwa.

“Kwa miundombinu iliyonayo Azam hata ikinolewa naye, Juma Mgunda au Selemani Matola wanaweza kuifikisha mbali ikiwemo kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara nyingine kwani ina kila kinachohitajika.

"Mimi siogopi kusema ukweli maana naona Azam ina kila kitu, lakini haifanyi vizuri kwa kuwa watu wanaopewa majukumu kuivusha hawawezi, wawape timu watu sahihi ambao wanaujua utendaji lakini wao wanapeana kazi kishkaji ndicho kinachowafelisha.

"Wachezaji wanaosajiliwa (Azam FC) ni kama hawajitambui na wamekuwa wakiridhikia na pesa nyingi wanazolipwa kwa vile hawana presha wanayopewa kuwafanya wapambane"

"Kwa wanavyocheza uwanjani ukiitazama na Yanga iliyoweka kambi Avic Town Dar es Salaam na Azam iliyotumia pesa nyingi kwenda Tunisia utaona vitu viwili tofauti.

"Yaani Yanga utasema wao ndio walikuwa nje ya nchi kutokana na ubora wa soka wanalocheza kumbe hapana, ila hawa waliosafiri kambi ya wiki mbili, lakini wanapoteza muda mwingi njiani kwenye safari ni lazima wabadilike," amesema Julio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live