Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji hawa hawawezi kuipeleka Simba nusu fainali - Mchambuzi

Simba Tizi La Mwisho Dar Wachezaji hawa hawawezi kuipeleka Simba nusu fainali - Mchambuzi

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid 'Wakanda Republic' amesema kuwa Klabu ya Simba ilijiwekea malengo ya kufika nusu fainali ya CAFCL msimu huu lakini uwezo wa wachezaji wao unaonyesha hawawezi kutekeleza malengo hayo.

Wakanda amesema hayo kufuatia mwendelezo wa matokeo mabovu ambao kikosi cha Simba kimekuwa kikiyapata kwa siku za hivi karibuni.

"Sehemu muhimu ambayo tulifeli ni sehemu ya maandalizi, inawezekana kikosi cha Simba matatizo yao yamekwisha zungumzwa sana, haswa haswa eneo la usajili kuelekea mashindano ya kimataifa.

"Na target walizojiwekea, ukiweka target za kwenda nusu fainali sajili wachezaji ambao wana hadhi ya kukupeleka nusu fainali, ukiweka target za kufika hatua ya makundi sajili wachezaji ambao wana hadhi ya kukufikisha hatua ya makundi

Simba waliweka-target za kufika nusu fainali.

"Lakini uhalisia wa kikosi chao ni wa hatua za makundi ambao ndiyo wapo hivi sasa, performance yao kwenye hizi mechi mbili walizocheza iko wazi watu wote wameziona performance ambazo kwenye standard ya Simba haziridhishi," amesema Wakanda Republic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live