Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji chanzo cha kuondoka Barbara Msimbazi

FjeSOxIWYAMdxYW Wachezaji watajwa CEO kung'atuka Simba SC

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku cheche tangu CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez atangaze kuachia wadhifa huo ifikapo Januari 2023, Taarifa za chini chini kutoka ndani ya klabu ya Simba juu ya sakata la kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez zinadai kuna Wachezaji walipiga kura ya siri kumkataa mwanamama huyo.

Inadaiwa Barbara alifanya mambo yafuatayo akiwa katika nafasi yake kama Mtendaji Mkuu;

Wachezaji wa Simba SC walipiga kura ya maoni na wengi walichagua CEO huyo aachie ngazi. Inadaiwa Barbara aliondoa baadhi ya posho ndani ya klabu hiyo.

Mwanamama huyo anadaiwa kuongeza matumizi na shughuli binafsi. Barbara alikuwa hataki wachezaji kumtembelea hata kwa shida binafsi.

Simba imepoteza wachezaji na makocha wazuri chini ya Afisa Mtendaji huyo kwa kwanza Mwanamke katika historia ya vilabu Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live