Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Yanga waahidi ushindi Ghana

Yanga Tizi Ghana Wachezaji Yanga waahidi ushindi Ghana

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Young Africans kimeonesha kuwa na malengo ya kupambana ili kuhakikisha kinashinda mchezo dhidi ya Medeama ya nchini ya nchini Ghana ili kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2023/24.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakaopigwa keshokutwa Ijumaa (Desemba 08) saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Young Africans imetua Ghana, ikiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi, baada ya kutoka kudroo bao 1-1 dhidi ya Al Ahly na kabla ya hapo walifungwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria ambao ulikuwa mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza.

Nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa bado hawajapoteza matumaini ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo kimahesabu kutokana na idadi ya michezo waliyoibakisha.

Mwamnyeto amesema kuwa wanakwenda kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo na kutokana na maandalizi, mikakati waliyoipanga Wachezaji, Benchi la Ufundi na Viongozi wanaona watafanya vizuri mbele ya wenyeji wao Medeama.

“Kila mchezaji anauhitaji mchezo huu dhidi ya Medeama, na hakuna kitu kingine tunachokihitaji zaidi ya ushindi ambao utatuwekea mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuatia,” amesema Mwamnyeto.

Naye Nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job amesema kuwa: “Tuna kibarua kigumu katika mchezo huu dhidi ya Medeama ambao umebeba matumaini yetu makubwa ya kufuzu hatua inayofuata, kuelekea mchezo huu tunahitaji ushindi pekee.”

Na kiungo mkabaji wa timu hiyo, Khalid Aucho amesema kuwa: Maandalizi tunayoyafanya yanatosha kwetu sisi wachezaji kupata pointi tatu tutakapocheza dhidi ya Medeama, kwani ushindi utatuongezea hamasa ya sisi kupambana katika michezo ijayo. Kikubwa maashabiki watuombe dua ili tupate ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live