Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Yanga kulamba Sh200 milioni wakiifunga Simba SC

98074 Yanga+pic Wachezaji Yanga kulamba Sh200 milioni wakiifunga Simba SC

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uongozi wa Yanga na mdhamini GSM wamehaidi kutoa Sh 200milioni kwa wachezaji wa Yanga iwapo watashinda mechi yao dhidi ya Simba Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza makao makuu ya Yanga, Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema wadhamini wa GSM wameweka mezani Sh200 Milioni kwa wachezaji endapo watapata ushindi wa aina yoyote siku hiyo.

"Hata wakichukua ubingwa sio tatizo, tunachohitaji ni kuwachapa, nadhani raha ya ubingwa utakuwa umeisha na kuwanyamazisha kupiga kelele hovyo mtaani.

"Tulikuwa na utaratibu wa kutoa motisha kila wanaposhinda kwenye michezo ya Ligi Kuu hupewa Sh 10Milioni, lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa Jumapili tumeamua kufanya kitu kwa wachezaji ili kuweka raha Jangwani,' alisema Nugaz.

Aliongeza kocha, Luc Eymael amemweleza kuwasoma Simba kwa muda mrefu tangu alipowasili nchini kukinoa kikosi hicho na amegundua mambo mengi ya kuwadhibiti wapinzani wao.

"Luc ameniambia atashambulia mwanzo mwisho kwa kasi, tofauti na michezo iliyopita kwani, Boniface Mkwasa (kocha Msaidizi wa Yanga) amemweleza vitu vingi kuhusu mchezo huo."

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz