ARSENAL iko tayari kuwauza wachezaji tisa iliwapate fedha kwa ajili ya kumpa nguvu KochaMikel Arteta ya kushusha jembe lingine kikosini hapo.
The Gunners wametumia mkwanja mkubwamsimu huu wa joto ili kushindana kusaka ubingwa wa Premier ambao msimu uliopitawaliukosa dakika za mwisho mbele ya Manchester City.
Arsenal wametoa pauni 105m kwa Declan Rice, pauni 65m kwa Kai Havertz na pauni 36.5m kwa Jurrien Timber, kwa matumaini wanaweza kumaliza miongo miwili ya kusubiri taji la ligi.
Kufikia sasa, walioondoka kikosini hapo ni nahodha wa zamani Granit Xhaka, aliyetua Bayer Leverkusen kwa pauni milioni 21.4, huku mauzo ya Pablo Mari, Matt Turner na Auston Trusty pia yakizidisha hazina.
Kocha Arteta anahitaji zaidi ya pauni milioni 100 ili kuendelea kuisuka timu yake na tayari amewaruhusu wachezaji tisa kuwekwa sokoni.
Nyota hao waliopo sokoni ni Folarin Balogun, Gabriel Magalhaes, Kieran Tierney, Takehiro Tomiyasu, Albert Sambi Lokonga, Rob Holding, Cedric Soares, Nicolas Pepe na Nuno Tavares hivyo wanaweza kusepa kabla ya Septemba 1.