Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Prisons waitisha Simba

Prisons+piv Wachezaji Prisons waitisha Simba

Sun, 18 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIVER ALBERT NA OLIPA ASSA SIMBA ina kibarua kizito mbele ya Prisons timu hizo zitakapokutana Alhamis ijayo kwani kikosi cha wajelajela hakina masihara kinapocheza uwanja wa nyumbani.

Hata hivyo, Simba inaweza kupata wepesi kutokana na uchovu ambao watakuwa nao Prisons kwani hawatakuwa wamepata muda wa kupumzika baada ya kutoka kucheza na JKT Tanzania mjini Dodoma.

Prisons itaikabili JKT Tanzania kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na baada ya mchezo itasafari kurudi Sumbawanga kucheza na Simba Alhamisi.

Licha ya wachezaji wa Prisons kulalamikia ratiba inawabana na kuwachosha, lakini wamesema watapambana kiume ili kuvuna pointi tatu.

Rekodi zinaonyesha Simba imekuwa ikipata wakati mgumu inapoikabili Prisons kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya, lakini hivi sasa maafande hao wamehama na wanatumia Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Katika mechi mbili za msimu huu ambazo Prisons imecheza kwenye uwanja huo imeshinda moja dhidi ya Namungo kwa bao 1-0 na imepoteza moja dhidi ya Azam kwa bao 1-0. Katika mchezo dhidi ya Azam, Prisons ilicheza kwa kiwango bora lakini ikajikuta ikiruhusu bao dakika ya 89.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz