Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Man United walalamikia jezi

Wachezaji Man UNited Wachezaji Man United walalamikia jezi

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inadaiwa kuwa wachezaji wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, wanalazimika kuvaa ‘jezi’ zisizo rasmi wakati wa ‘mechi’ kutokana na ‘jezi’ zilizotengenezwa na #Adidas, kuwabana sana.

Kufuatia malalamiko hayo, kampuni ya Adidas imeanza kutafuta suluhu ya haraka baada ya baadhi ya wachezaji kuacha kuvaa ‘soksi’ rasmi tangu mchezo wa pili wa msimu huu, dhidi ya Tottenham wakilalamika kuwa zilikuwa zikiwabana sana maeneo ya nyuma ya miguu (Vigimbi).

‘Golikipa’ wa ‘timu’ hiyo, Andre Onana, aliacha kuvaa ‘jezi’ hizo rasmi kwa ajili ya wachezaji na kuhamia kwenye jezi zilizotengenezwa kwa ajili ya mashabiki, kuanzia kwenye ‘mechi’ dhidi ya Sheffield United, Oktoba 2 mwaka huu.

Hata hivyo inadaiwa kuwa baadhi ya wachezaji wamelazimika kukata matobo nyuma ya ‘soksi’ zao kama suluhisho la muda, lakini inaonekana kuwa hivi sasa wameanza kuvaa soksi zilizotengenezwa kwa ajili ya mashabiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live