Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Mamelodi waliodaiwa kuumia wawasili Timu ya Taifa

Mamelodi Ms Wachezaji Mamelodi waliodaiwa kuumia wawasili Timu ya Taifa

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa klabu ya Mamelodi Sundowns waliodaiwa kuwa majeruhi wamewasili kwenye kambi ya timu ya taifa ya Afrika Kusini iliyopo Algeria.

Shirikisho la soka Afrika Kusini -SAFA-liliwataka wachezaji wote saba wa Mamelodi Sundowns kwenda kwenye timu ya taifa kufuatia kocha wa timu hiyo, Hugo Broos kulalamika kuwa kocha wa Mamelodi amedai kuwa baadhi ya wachezaji ni majeruhi.

Kocha wa Sundowns Rhulani Mokwena alidai kuwa kipa Ronwen Williams, Themba Zwane na Teboho Mokoena hawako kwenye hali nzuri kuweza kucheza.

Kocha wa Bafana, Broos alikasirishwa na kitendo cha Mokwena kuzungumza na wanahabari kuhusu majeruhi badala ya kuwasiliana na madaktari wa timu ya taifa.

Bafana Bafana watacheza mechi mbili za kirafiki na Andorra (Alhamisi) na Algeria (Jumanne).

Mamelodi Sundowns kwa upande wao wana kibarua cha kuikabili Yanga ya Tanzania katika michuano ya Mabingwa Afrika Machi 30.

Wachezaji wa Sundowns walioitwa Bafana Bafana ni:

◉ Teboho Mokoena

◉ Ronwen Williams (GK)

◉ Thapelo Morena

◉ Themba Zwane

◉ Grant Kekana

◉ Terrence Mashego

◉ Aubrey Modiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live