Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Majimaji watimuliwa hotelini Dar

MAJIMAJI MSS Wachezaji Majimaji watimuliwa hotelini Dar

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Majimaji ikitarajia kushuka uwanjani leo kucheza dhidi ya Dar City katika mwendelezo wa First League, timu hiyo imewaangukia wadau ikiomba msaada ili kulipa deni katika hoteli waliyofikia na kuweza kusafiri kurudi mjini Songea.

Bingwa huyo wa zamani wa kombe la Muungano (1999) imeelezwa amekwama Dar es Salaam baada ya kutimuliwa kwenye hoteli waliyofikia kwa deni la Sh398,000.

Mjumbe wa bodi ya timu hiyo, Catherine Masasi amesema tangu walipomaliza mchezo wao uliopita dhidi ya African Lyon walipofungwa 5-2 timu iliendelea kubaki jijini humo huku ikikabiliwa na changamoto nyingi licha ya kuvumilia.

Amesema kwa siku tatu mfululizo wachezaji 13 na viongozi watatu wamelala nje baada ya kufukuzwa hotelini kwa deni hilo na kwamba hata leo hawajajua muafaka wao na kuomba wadau kuisaidia.

"Hadi sasa deni ni Sh398,000 japokuwa hatujajua tunaondoka lini na kwa usafiri upi, hakuna chakula wala kitu chochote hatujawasiliana na mamlaka yoyote japokuwa tulikuwa na wazo la kuwatafuta Bodi ya Ligi ili tuone wanatusaidiaje," amesema Catherine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live