Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Italia walivyokosa magari ya Benito Musolin

Eng Vs It Wachezaji Italia walivyokosa magari ya Benito Musolin

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 1934, November 14, uwanja wa Arsenal, kipindi hicho unaitwa Highbury ulikuwa mwenyeji wa mchezo mkubwa wa kirafiki wa soka Barani Ulaya kati ya Italy dhidi ya England, kwa kipindi hicho Italy ndio walikuwa mabingwa wa Dunia na England waliaminika kuwa na kikosi bora zaidi lakini hawakushiriki kwenye fainali za kombe la Dunia kwa kipindi hicho.

Mchezo huo uliitwa Battle of Highbury kutokana na ubora wa kikosi cha kila timu, mchezo ambao uliamuliwa na mwamuzi Otto Olsson kutoka nchini Sweden, ulihudhuriwa na watazamaji 56,044.

Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza ya Italy toka walipobeba ubingwa wa kombe la Dunia mwaka 1934, na England haikushiriki baada ya Chama cha soka cha England FA kujitoa kama mwanachama wa FIFA 1928.

England bado ilikuwa inaaminika kuwa na kikosi bora kwa kipindi kile, wengi waliamini mchezo huo ndio ulitakiwa kuwa mchezo halisi wa Fainal za kombe la Dunia licha ya kuwa ulikuwa mchezo wa kirafiki.

Mchezo ulikuwa muhimu zaidi kwa timu ya Taifa ya Italia kwani walikuwa wameahidiwa kila mchezaji kupatiwa gari aina ya Alfa Romeo na Rais wa kipindi hicho wa Italia Benito Mussolini, kwa kipindi hicho gari hiyo ilikuwa na thamani ya £150 kama wakiifunga England.

Hii ilikuwa ni mechi ya kipekee, na ndio ilikuwa mechi pekee iliyohusisha wachezaji saba wa Arsenal kwenye kikosi cha England.

Kwenye mchezo huo kulishuhudiwa ajali mbaya ya kuvunjika kwa mguu wa beki wa Italy Luis Mont baada ya kukumbana na Drake mchezaji wa England, aliendelea kucheza hivyo hivyo lakini baada ya dakika 15 alitoka uwanjani. Kwa kipindi hicho hapakuwa panaruhusiwa kufanya mabadiliko hivyo Italy ilibaki pungufu.

Mchezo huo ulimalizika kwa England kuibuka na ushindi wa goli 3-2, Wachezaji wa Italy wakakosa Magari.

Nikipata muda nitakuja kuwaeleza ilikuwaje baada ya wachezaji wa Italy kufika nchini Italia baada ya kupoteza mbele ya England, nini kilifuata patamu hapo...

Chanzo: www.tanzaniaweb.live