Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uhispania wamethibitisha kupitia taarifa yao kuwa hawatarejea tena kuichezea nchi hiyo kwenye mechi zijazo hadi pale hatua zitakapochukuliwa zaidi.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uhispania wamethibitisha kupitia taarifa yao kuwa hawatarejea tena kuichezea nchi hiyo kwenye mechi zijazo hadi pale hatua zitakapochukuliwa zaidi. Licha ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa kikosi hicho na kujiuzulu kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Hispania, Luis Rubiales ambaye alimbusu mchezaji, wachezaji hao wamesema bado hawaoni kama kurejea tena kuichezea Uhispania itakuwa salama kwao na wanataka hatua zaidi zichukuliwe.