Imeripotiwa kuwa viongozi na wachezaji klabu ya Gor Mahia waliibiwa simu zinazokadiriwa kuwa na gharama ya zaidi ya ksh 40,000 kwenye uwanja wa kasarani ambapo walikuwa na mchezo dhidi ya Nairobi city hapo Jumapili.
wizi huo ulifanyika kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya timu hiyo ambapo inaelezwa kuwa huenda wezi waliingia vyumbani kupitia dirisha ambalo lilibainika kuwa wazi kwani milango hufungwa wakati mchezo unaendelea.
Polisi wamesema kuwa jana jumatatu wangekuwa na majibu ya wahusika wote wa uhalifu huo kwani watatumia camera za ulinzi za uwanjani hapo kuwabaini.
Hii si mara ya kwanza tukio kama hili liliwahi kutokea pia uwanjani hapo kwani wachezaji na viongozi wa city stars waliwahi kuripoti kuibiwa pesa pamoja na vitu vyao mbalimbali kwenye uwanja wa Kasarani.
katika mchezo huo Gor mahia walipata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Nairobi city stars.