Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Chelsea simanzi kutimuliwa kwa Graham Potter

Potter Simanzi Wachezaji Chelsea simanzi kutimuliwa kwa Graham Potter

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa muda wa Chelsea Bruno Saltor amesema wachezaji wa klabu hiyo watakuwa kwenye huzuni kufuatia taarifa za kufutwa kazi kwa kocha mkuu Graham Potter.

Saltor (42) raia wa Uhispania kwa sasa anakiandaa kikosi hicho kuelekea mchezo wa Ligi kuu England dhidi ya Majogoo, Liverpool siku ya Jumanne.

Chelsea ilimfuta kazi Graham Potter kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Aston Villa na kumfanya Meneja huyo raia wa England kuwa kocha wa 13 kufungishwa virago mpaka sasa msimu huu.

Mkufunzi Julian Nagelsmann ambaye naye alioneshwa mlango wa kutokea wiki iliyopita huko Bayern Munich anahusishwa na kuchukua mikoba ya Potter huko darajani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: