Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji 6 JKT Queens waondoka kikosini

JKT Queens Players Wachezaji 6 JKT Queens waondoka kikosini

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JKT Queens wapo nchini Ivory Coast kwaajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa upande wa Wanawake wakiwa ni wawakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki, tayari wamecheza michezo miwili hatua ya Makundi, wakishinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja, huku wakisubiri mchezo wa leo dhidi ya CS Casablanca ili kuijua hatma yao kama wataendelea ama safari yao iishie hapo.

Kuelekea katika mchezo wa kesho baadhi ya nyota wa klabu hiyo wameondoka kambini na kurudi nchini kwaajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa wanawake chini ya miaka 20 ambao wana kibarua dhidi ya Nigeria Jumapili cha kutafuta tiketi ya kufuzu fainali ya kombe la Dunia.

Baada ya kutokea hili kocha wa timu ya Taifa na mshauri wa timu ya JKT Queens, Bakari Shime amesema hakutakuwa na athari yoyote kwa JKT Queens baada ya kuondoka wachezaji hao kuelekea mchezo wa leo kwani walikuwa wameshajiandaa tayari kwa hili na nyota waliobaki wanaweza kupambana na kupata matokeo yatakayo wafanya wafuzu hatua ya nusu fainali.

Pia Bakari amesema punde tu baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu ya Taifa Jumapili hii nyota hao watasafiri kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya kuungana na wengine kuelekea mchezo wa nusu fainali kwani timu hiyo itakuwa tayari imefuzu.

JKT Queens itashuka dimbani leo majira ya saa tano usiku kuikabili Club Sporting Casablanca ya Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live