Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji 5 wenye kiwango bora zaidi kwa sasa Duniani

Mbappe Haaland Psg City Wachezaji 5 wenye kiwango bora zaidi kwa sasa Duniani

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa 2022-23 ulianza kote Ulaya Agosti mwaka huu. Na dirisha lingine la kufurahisha la uhamisho wa majira ya joto lilifungwa Septemba Mosi na tunajua kwa hakika kwamba huu utakuwa ni msimu bora zaidi kwa soka duniani.

Baadhi ya timu kuna wachezaji tayari wameweka alama kwa ajili ya changamoto katika nyanja zote za msimu huu. Mfumo wa msimu wa mapema ni muhimu sana kwani huweka sauti kwa kampeni iliyosalia na huboresha hali ya kujiamini ya mchezaji mara mambo yanapoanza kuwa makali zaidi.

Bila kuchelewa zaidi, hebu tuangalie wachezaji watano walio katika kiwango bora zaidi duniani kwa sasa.

#5. Aleksandar Mitrovic (Fulham)

Aleksandar Mitrovic amekuwa na mwanzo wa kushangaza kwa mwezi wake wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia pia alikuwa katika kiwango kizuri cha ufungaji katika mwaka uliopita pia. Amefunga mabao 49 katika mechi 49 zilizopita za ligi akiwa na Fulham.

Mitrovic anajiamini kwa sasa na amefunga mabao sita katika mechi sita katika msimu wa Ligi Kuu England. Amesajili mikwaju 27 kwenye Ligi Kuu England hadi sasa msimu huu na hiyo ndiyo mikwaju mingi zaidi ya mchezaji yeyote kwenye ligi.

Hili halionyeshi tu njaa ya Mitrovic bali pia ni straika ambaye ana uwezo wa kuingia kwenye nafasi nzuri mara kwa mara ili kupata mkwaju wake. Kiwango cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, kimekuwa muhimu kwa Fulham kukaa katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya mechi sita.

#4. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)

Safu nzima ya ushambuliaji ya Paris Saint-Germain imekuwa katika hali nzuri msimu huu mpya. Baada ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kipindi cha majira ya joto, Kylian Mbappe ameanza kufanya kazi ya kushikilia ubavu wake kwa kuwa katika kiwango cha kuvutia.

Kasi yake ya kusisimua, uelekevu na harakati zake za kiakili humfanya aonekana mtu muhimu sana kwenye safu ya watatu ya kushambulia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao saba katika mechi sita za Ligue 1 hadi sasa msimu huu na anaonekana kuwa na kampeni kubwa zaidi.

#3. Lionel Messi (Paris Saint-Germain)

Lionel Messi hatimaye ameanza kufurahia maisha pale Paris. Baada ya kampeni mbaya ya kwanza akiwa na Paris Saint-Germain, Messi anatamba kwenye viunga vya Parc des Princes msimu huu. Uamuzi wa kocha mpya, Christophe Galtier kumhamisha Messi kwenye nafasi muhimu zaidi umefanya maajabu kwa mchezaji na timu.

Mshindi huyo mara saba wa Ballon d'Or anatumika kama kiungo mshambuliaji msimu huu. Hii imeisaidia PSG kutumia vema uwezo wa ajabu wa uchezaji wa Messi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, amekuwa kiungo kati ya safu ya kiungo na ushambuliaji na amefanya kazi nzuri hadi sasa.

Katika mechi sita za Ligue 1 hadi sasa msimu huu, Messi amefunga mabao matatu na kutoa asisti tano.

#2. Erling Haaland (Manchester City)

Wakati Erling Haaland akijiunga na Manchester City, kulikuwa na wasiwasi kama angekuwa anafaa kwa kikosi cha Pep Guardiola. Imemchukua Haaland mwezi mmoja kuwanyamazisha wakosoaji wake.

Mshambulizi huyo wa Norway ameingia kwenye ndoto kamili ya kuanza maisha katika Ligi Kuu. Amefunga mabao 10 na kutoa asisti moja katika mechi sita kwenye Ligi Kuu England hadi sasa msimu huu.

Haaland alifunga ‘hat-trick (mabao matatu) mfululizo katika mechi yake ya nne na ya tano ya Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace na Nottingham Forest.

Anaonekana kila kukicha mnyama mkubwa ambaye alitikisa kabisa Bundesliga katika misimu michache iliyopita. Hakuna shaka kwamba yeye ndiye kitu kikubwa kinachofuata kwenye soka.

#1. Neymar Jr. (Paris Saint-Germain)

Neymar Jr. hakushiriki sana kwa PSG katika msimu wa 2021-22 kutokana na matatizo mengi ya majeraha. Hata alizomewa mara nyingi na mashabiki wa kikosi hicho chenye maskani yake pale Parc des Princes baada ya timu hiyo kuondolewa katika raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa na mwanzo mzuri sana wa msimu huu. Neymar amekuwa moto kwa PSG msimu wa 2022-23 hadi sasa. Amekuwa akijawa na kujiamini na ameonekana kutisha.

Huku Messi akicheza nyuma yake, Neymar ametumia muda mwingi kwenye safu ya ushambuliaji na huko ndiko kwenye hatari yake zaidi. Mbinu yake ya kupendeza, akili na harakati zimemfanya aonekane kutozuilika hadi sasa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amefunga mabao saba na kutoa pasi za mabao sita katika mechi sita za Ligue 1 hadi sasa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live