Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji 28 Yanga wanaoenda Morocco

BRYSON DAVID YANGA Miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga, David Bryson

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabingwa wa Kihistoria Klabu ya Yanga itaondoka Nchini siku ya Jumapili na nyota wake kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/2022.

Yanga itaondoka na msafara wa wachezaji 28 katika safari hiyo na itakuwa kwa siku zisizozidi 10,kwa mujibu wa Afisa habari wao Hassan Bumbuli, wakiweka kambi katika Akademi ya soka ya Mohammed VI ambapo ndani kuna majengo makubwa ya kiutawala, hospitali, viwanja vinne vya mazoezi vya kisasa vya nyasi bandia na nyasi asilia vyenye ukubwa tofauti.

Kuna mabwawa ya kisasa, kumbi za chakula na mikutano pamoja na vyumba vya malazi vyenye hadhi ya hoteli ya nyota tano. Viwanja vyote vinne kila kimoja kina urefu wa Mita 105 na upana wa Mita 68 lakini muna kingine kidogo cha mraba ambacho kina urefu wa mita 48.

Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2009 na uzinduzi rasmi ulikuwa 2010 na ulifanywa na Mfalme Mohammed wa Sita aliyefadhili gharama za ujenzi ikiwa ni miongoni mwa miradi aliyoianzisha kwa lengo la kuinua maendeleo ya Morocco

Kiujumla gharama za ujenzi wa kituo hicho ni kiasi cha Dinari 140 milioni sawa na karibu Sh36 bilioni.

Baadhi ya nyota waliozalishwa na kituo hicho ni Youssef En-Nesyri [Leganes], Hamza Mendyl [FC Schalke] na Ahmed Reda Tagnaouti [Wydad Casablanca]

Msafara wa Yanga utawajumuisha makipa wote watatu, Diarra Djigui (Mali), Erick Johora na Ramadhan Kabwili.

Mabeki ni Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Adeyum Saleh, Paul Godfrey, huku wapya ni; mzawa David Bryson, Djuma Shaban na Yannick Bangala wote kutoka DR Congo.

Kujumuishwa kwa Djuma utapunguza presha za mashabiki wa Jangwani baada ya maneno kuwa, beki huyo ameikacha timu hiyo na alikuwa akienda Uarabuni habari ambazo mabosi wa GSM wanaomwaga fedha kuisajilia timu hiyo walicheka walipozisikia.

Viungo ni; Deus Kaseke, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Mapinduzi Balama, Mukoko Tonombe, ingizo jipya Khalid Aucho (Uganda).

Washambuliaji ni; Farid Mussa, Ditram Nchimbi, Yacouba Sogne, Said Ntibazonkiza, wapya wakiwa wazawa Yusuf Athuman, Dickson Ambundo, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Jesus Moloko wote kutoka DR Congo.

Hata hivyo Waziri Junior na Said Makapu hawamo katika orodha hiyo, taarifa zikisema hawatakuwa sehemu ya kikosini msimu ujao licha ya kufanywa siri.

Msafara huo pia utawajumuiisha viongozi 9 wa benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Nesreddin Nabi na wasaidizi wake, Shir Hammadi, Jawad Sabri na Razack Siwa, meneja Hafidh Saleh, watunza vifaa Mahmoud Omary, Mohamed Mposo, Daktari Shecky Mngazija, Mtaalam wa misuli Jacob Onyango na viongozi sita wa klabu.

Yanga yenye sura nyingi mpya inajiandaa kwa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza Septemba 11.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz