Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji 22 wa Simba wawafuata Waarabu Libya

Wachezaji 22 Wa Simba Wawafuata Waarabu Libya.png Wachezaji 22 wa Simba wawafuata Waarabu Libya

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji 22 wa Simba wamesafiri Jumatano, alfajiri Septemba 11 kwenda Libya kwa ajili ya mechi ya ugenini ya raundi ya pili ya Kombe la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli itakayochezwa kwenye Uwanja wa Juni 11, Tripoli Libya.

Msafara huo wa Simba umeanzia safari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa usafiri wa ndege ya Shirika la Uturuki hadi Istanbul ambako utalala na Alhamisi asubuhi utaelekea Tripoli.

Kocha Fadlu Davids wa Simba ameonekana kuamua kwenda na kundi kubwa la viungo ambao wako tisa, mabeki wakiwa saba huku akijumuisha makipa watatu na washambuliaji watatu.

Kikosi hicho kimewaweka kando wachezaji wawili kutokea kikosi cha vijana ambao walikuwepo benchi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Tabora United na Fountain Gate, Okech Nyembe na Daruwesh Rashid lakini pia hayupo kipa Abel Hussein.

Pia kikosi hicho hakitokuwa na Hussein Kazi, Ladack Chasambi na Salehe Karabaka.

Makipa watakaosafiri ni Mousa Camara, Aishi Manula na Ally Salim na washambuliaji ni Valentino Mashaka, Steven Mukwala na Leonel Ateba.

Viungo ambao watasafiri ni Augustine Okejepha, Charles Ahoua, Debora Fernandes, Awesu Awesu, Kibu Denis, Fabrice Ngoma, Yusuph Kagoma, Joshua Mutale na Edwin Balua.

Mabeki ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Chamou Karabou, Kelvin Kijiri, Abdulrazack Hamza, Che Fondoh Malone na Valentine Nouma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live