Wakati mashindano ya mataji yanajaribu mishipa ya mchezaji, soka la ligi ni kuhusu uthabiti. Katika kipindi cha msimu wa kuchosha, wanasoka huwekwa mbele ya timu zilizo na sifa tofauti, uwezo na mitindo tofauti ya kucheza. Ni wale tu walio wakali zaidi na wanaoweza kubadilika zaidi na wataweza.
Leo, tutaangalia baadhi ya washambuliaji bora ambao wamekuwa na kiwango bora cha kuvutia tangu mwaka 2020. Hapo chini kuna wafungaji 10 bora ambao wamefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi tangu mwaka 2020, twende sasa...
#10. Lionel Messi - mabao 56
Mchezaji nyota wa Paris Saint-Germain (PSG), Lionel Messi amefunga mabao 56 katika michezo 96 ya ligi tangu mwaka 2020.
Messi, ambaye aliisaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia la FIFA la 2022 Desemba mwaka jana, alifunga mabao 25 kwenye Ligi Kuu Hispania, LaLiga, msimu wa 2019-20, na kushinda Kiatu cha Dhahabu ‘Pichichi Trophy’. Kati ya jumla ya mabao yake, alifunga 12 mwaka 2020.
Katika msimu wa 2020-21, Messi alifunga mabao 30 katika mechi 35 za LaLiga. Barcelona haikushinda taji la Hispania, lakini Messi alishinda tuzo ya Pichichi. Msimu uliofuata, akiwa PSG, Messi alifunga mara sita pekee katika mechi 26 za Ligue 1 huku klabu hiyo ikishinda taji la Ligi Kuu Ufaransa.
Msimu huu, amekuwa mzuri zaidi, tayari amefunga mabao nane na kutoa asisti 10 katika mechi 15.
#9. Wissam Ben Yedder - mabao 61
Mshambuliaji wa kati wa AS Monaco, Wissam Ben Yedder amefunga mabao 61 katika michezo 100 ya ligi tangu mwaka 2020, akiibuka mfungaji bora wa timu hiyo ya Ufaransa kwenye Ligue 1.
Ben Yedder, aliyejiunga na Monaco Julai 2019, alifunga mabao 18 katika michezo 26 ya Ligue 1 katika msimu wake wa kwanza. Mabao matano kati ya hayo yalikuja katika nusu ya pili ya msimu wa 2019-20. Msimu uliofuata, alifunga mabao 20 katika michezo 37 na kuisaidia Monaco kumaliza katika nafasi ya tatu. Katika msimu wa 2021-22, Ben Yedder alirekodi kurejea kwake kwa mabao 25 katika mechi 37.
Ben Yedder amefurahia mwendo mzuri wa Ligue 1 msimu huu pia, akifunga mara 11 na kutoa asisti mbili katika mechi 16.
#8. Mohamed Salah - mabao 62
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, amefunga mabao 62 katika mechi 108 kwenye soka la Uingereza tangu 2020.
Katika msimu wa 2019-20, Salah alifunga mara 19 katika mechi 34 huku Liverpool ikishinda taji lao la 19 la ligi. Mabao yake kumi kati ya 19 alifunga katika kipindi cha pili cha msimu wa 2019-20, mwaka 2020. Msimu uliofuata, Salah alifunga mara 22 katika mechi 37. Aliboresha idadi yake msimu wa 2021-22, akiingia akiwa na mabao 23 katika michezo 35 huku 'Wekundu' hao wakipoteza mbio za ubingwa kwa Manchester City kwa pointi moja pekee.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri msimu huu amefunga mabao saba pekee na kutoa pasi nne za mabao katika mechi 18 alizocheza hadi sasa.
#7. Harry Kane - mabao 62
Mchezaji nyota wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amekuwa mmoja wa washambuliaji bora kwenye Ligi Kuu England, huku akifunga mabao 62 katika mechi 101 tangu 2020.
Kane alifunga mabao 18 ya ligi katika mechi 29 msimu wa 2019-20, huku saba kati ya msimu huo akifunga 2020. Msimu uliofuata, alifunga mabao 23 katika michezo 35, akishinda Kiatu cha Dhahabu. Msimu wa 2021-22, Kane alianza polepole, lakini akaongeza kasi katika raundi ya pili na kumaliza na jumla ya mabao 17 katika michezo 37.
Kane ameonekana kuwa mkali zaidi msimu huu, akifunga mara 15 katika mechi 17 kwenye Ligi Kuu England.
#6. Karim Benzema - mabao 67
Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Karim Benzema, ameibuka kuwa hirizi ya klabu hiyo katika zama za baada ya Cristiano Ronaldo. Tangu Januari 2020, Mfaransa huyo amefunga mara 67 katika mechi 95 za LaLiga.
Katika msimu wa 2019-20, Benzema alifunga mara 21 na kutoa asisti nane katika michezo 37 huku Real Madrid ikishinda LaLiga. Mabao yake tisa katika msimu wa 2019-20 wa LaLiga alifunga mwaka 2020. Msimu uliofuata, Benzema alifunga mabao 23 na kutoa asisti tisa katika mechi 34 za LaLiga, lakini Madrid walishindwa kutwaa taji, huku Atletico Madrid wakitwaa ubingwa huo.
Msimu wa 2021-22 uliashiria msimu bora zaidi wa kazi ya Benzema. Alifunga mabao 27 na kutoa asisti 12 katika michezo 32 huku 'Los Blancos' hao wakishinda LaLiga. Mchezaji huyo wa zamani wa Kimataifa wa Ufaransa, ameonekana kuwa mkali msimu huu pia, akifunga mara nane na kutoa asisti katika mechi 9 za LaLiga hadi sasa.
#5. Cristiano Ronaldo - mabao 69
Ni nyota wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo alifunga mabao 69 katika michezo 93 ya ligi kwenye ligi tano bora za Ulaya kati ya Januari 2020 na Novemba 2023.
Nyota huyo wa Ureno alifunga mabao 31 katika mechi 33 za Serie A msimu wa 2019-20, huku mabao 21 kati ya hayo akifunga katika kipindi cha pili cha msimu, mwaka 2020. Juventus ilishinda taji la Serie A mwaka huo.
Msimu uliofuata, alifunga mabao 29 katika michezo 33, akishinda tuzo ya mfungaji bora, lakini akakosa taji la Serie A. Alijiunga tena na Manchester United msimu uliofuata na kufunga mabao 18 katika mechi 30 kwenye Ligi Kuu England.
Kwa bahati mbaya, mambo yalikwenda tofauti chini ya kocha Erik ten Hag msimu wa 2022-23, huku akiondoka kwenye klabu hiyo Novemba baada ya kufunga bao moja pekee katika mechi 10 za ligi.
#4. Ciro Immobile - mabao 73
Mshambuliaji wa Lazio, Ciro Immobile, amekuwa mchezaji anayeongoza Serie A muongo huu, akifunga mabao 73 katika mechi 101 za ligi.
Immobile alishinda tuzo yake ya kwanza ya mfungaji bora katika msimu wa 2019-20, akifunga mara 36 katika michezo 37. Mabao yake 19 ya kuvutia kati ya 36 yalipatikana katika kipindi cha pili cha msimu wa 2019-20.
Msimu uliofuata, matokeo ya Immobile yalishuka sana, huku akifunga mabao 20 katika michezo 35. Msimu uliopita, Immobile alionekana tena kama mfungaji bora akifunga mara 27 katika mechi 31.
Immobile, ambaye kwa sasa anauguza jeraha la misuli ya paja, amefunga mabao saba katika mechi 15 alizocheza msimu huu.
#3. Kylian Mbappe - mabao 75
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe, amekuwa moto sana kuwakabili walinzi wa Ligue 1, huku akifunga mara 75 katika mechi 91 za ligi tangu mwaka 2020.
Katika msimu wa 2019-20, Mbappe alifunga mabao 18 katika mechi 20. Alifunga mabao saba na kutoa asisti mbili katika kipindi cha pili cha msimu wa 2020-21, mwaka 2020. Alishinda tuzo ya mfungaji bora msimu huo.
Katika msimu wa 2020-21 wa Ligue 1, Mbappe alifunga mara 27 katika mechi 31. PSG walikosa taji la ligi, lakini Mbappe alihifadhi tuzo yake ya mfungaji bora. Msimu uliopita, Mbappe alifunga mara 28 katika mechi 35 na kushinda tuzo yake ya mfungaji bora kwa mara ya nne mfululizo na kuiwezesha PSG kutwaa taji la 10 la Ligue 1.
Msimu huu pia, Mbappe amekuwa katika hali nzuri. Akiwa amefunga mara 13 na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi 17.
#2. Erling Haaland - mabao 83
Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kwenye orodha hii, amefunga mabao 83 katika mechi 84 za ligi tangu 2020.
Haaland alijiunga na Borussia Dortmund kutoka RB Salzburg Januari 2020. Kati ya Januari na Juni, alifunga mara 13 katika mechi 15. Msimu uliofuata, alitikisa nyavu mara 27 katika mechi 28. Katika msimu wake wa mwisho akiwa Dortmund, Haaland alifunga mara 22 katika mechi 24 za Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga.
Haaland amekuwa katika daraja la aina yake kwenye Ligi Kuu England. Haaland amefunga mara 21 na kutoa asisti tatu katika michezo 17 ya Ligi Kuu England hadi sasa. Ilimchukua mechi 14 pekee kufikia mabao 20. Hakuna mchezaji katika historia aliyefikia hatua hiyo mapema namna hiyo.
#1. Robert Lewandowski - mabao 104
Akiwa amefunga mabao 104 katika mechi 92 tangu 2020, mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski yuko kileleni mwa orodha hii.
Lewandowski, ambaye alijiunga na Barca kutoka Bayern Munich majira ya joto yaliyopita, alifunga mara 34 msimu wa 2019-20, huku mabao 15 kati ya hayo akifunga 2020. Msimu uliofuata, alipanda daraja, akifunga mabao 41 katika mechi 29 pekee.
Hatimaye, katika msimu wa 2021-22, alifunga mara 35 katika michezo 34. Bayern Munich ilishinda taji la Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, katika misimu yote mitatu, huku Lewandowski akitwaa tuzo ya mfungaji bora katika kila msimu.
Ametikisa nyavu akiwa na Barcelona pia, ambapo hadi sasa anaongoza kwenye orodha ya wafungaji bora akiwa amefunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza.