Hivi karibuni kumekuwa na picha zinazosambaa sana zinazomuonyesha mchezaji wa Manchester City Kayle Walker akiwa anatoka na mwanamke ambaye si mkewe kwenye moja ya baa nchini England.
Hiyo imezua mjadala na inadaiwa hadi sasa hakuna maelewano baina yake na mkewe Annie Kilner kwani indaiwa kuwa hiyo sio mara ya kwanza jamaa amekuwa akichepuka mara kwa mara.
Lakini wakati wewe unashangaa haya Walker nikwambie tu kuna mastaa wengi wenye skendo hizo za kuchepuka na baadhi yao zimesababisha waachane na wake zao na wengine wakasamehewa. Leo tumekuletea baadhi ya mastaa waliowahi kukumbwa na skendo kama hizi na kilichotokea baada ya hapo.
WAYNE ROONEY
Staa huyu amekuwa na skendo nyingi kama yalivyo magoli aliyofunga uwanjani wakati anacheza soka.
Kwa alikuwa kwenye uhusiano wa tangu utotoni na Coleen ambaye kwa sasa ni mkewe. Lakini akiwa kwenye uhusiano huo mwaka 2004 gazeti la Sunday Mirror liliripoti kwamba Rooney alilipa Pauni 140 ili kulala na mrembo Charlotte Glover.,
Mwaka huo huo pia alitoka na Gina McCarrick, kisha akamlipa Pauni 45 na baadae akatoka na Patricia Tierney ambaye alikuwa na umri mkubwa kuliko yeye.
Hakuishia hapo Rooney alidaiwa kulipa zaidi ya Pauni 1000 ili kutoka na Jenny Thompson, kisha July 2009 akatoka pia na Helen Wood wakati ambao Coleen alikuwa ni mjamzito. Lakini licha ya matukio yote hayo Coleen alisamehe na wameendelea kuishi pamoja hadi sasa.
OLIVIER GIROUD
Mwaka 2014 wakati straika huyu wa kimataifa wa Ufaransa anaichezea Arsenal picha zilizokuwa zikimuonyesha yupo na boksa tu kwenye chumba kimoja cha hotel nchini England akiwa na mwana mitindo Celia Kay.
Baada ya hapo Giroud alikiri na kuomba msamaha mkewe ambaye wakati huo alikuwa amezaa naye watoto wanne, timu yake na mashabiki kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Mkewe aitwaye Jennifer alimsamehe na hadi sasa wameendelea kudumu kwenye ndoa ikiwa ni jumla ya miaka 11.
ANDY CARROLL
Hii ndio ilikuwa mbaya zaidi, picha za Andy Carroll akiwa kitandani na mwanamke huku akiwa hajielewi zilisambaa wiki mbili tu baada ya kumvisha pete mchumba wake Billi Mucklow.
Mwanamke ambaye alionekana kuwa kwenye picha hiyo ya kitandani pamoja na Carroll ni Taylor Jane Wilkey ambaye baadaye alikanusha na kudai kwamba hakukuwa na kitu chochote kilichotokea.
Baada ya hapo Andy na Billi aliyemvalisha pete walifanikiwa kufunga ndoa na wamedumu hadi leo.
RYAN GIGGS
Mwaka 2011, staa huyu wa zamani wa Manchester United alihusishwa kuwa alidumu kwenye uhusiano wa kimapenzi na mke wa kaka yake kwa miaka isiyopungua nane.
Wakati skendo hizi zinaripotiwa kwenye magazeti na televisheni mbali mbali staa huyu pia alikuwa anahusishwa kutoka kimapenzi na staa wa mashindano ya Big Brother Imogen Thomas.
Skendo hizi zilisababisha mkewe aondoke nyumnbani na kudai talaka ambayo aliipata mwaka 2017 akilipwa na fidia ya Pauni 40 milioni.
TIGER WOODS
Taswira na heshima ya staa huyu wa mchezo wa Golf ilichafuka sana mwaka 2009 baada ya kuibuka kwa moja kati ya skenedo kubwa zilizotikisa Dunia na hata ikababisha aachane na mkewe.
Kwa mujibu wa watu ambao walikuwa wakimsaidia kumtafutia wanawake ambapo mmoja wao alikuwa ni Michelle Braun alifichua kwamba kila mwezi staa huyo alikuwa akilala na wanawake zaidi ya 10 tofauti wakiwemo wanafunzi wa vyuo mbali mbali na wana mitindo na hadi kufikia mwaka huo inadaiwa alilala na wanawake wasiopungua 120.
Baada ya mambo hayo kufichuka mke wa Woods Elin Nordegren ambaye alikuwa amezaa naye watoto wawili alidai talaka na akalipwa fidia ya pesa inayokadiriwa kufikia Dola 100 milioni.
JOHN TERRY
Tetesi zilidai kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mchumba wa mchezaji mwenzake wa Chelsea na England Wayne Bridge aitwaye Vanessa Perroncel mwaka 2009.
Taarifa zilizua mtafaruku mkubwa na ikafikia hatua Bridge akakataa kumpa mkono Terry wakati wa mechi kati ya Chelsea na Manchester City. Hata hivyo mhusika mwenyewe Vanessa alikanusha kabisa kwamba yeye alikuwa kwenye uhusiano na Terry.
Bridge na Vanessa walianza uhusiano mwaka 2005 na wakafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume kabla ya kutengana mwaka 2009 na inadaiwa kuwa hata kuachana kwao kulisababishwa na Terry ambaye ndio alimshawishi Vanessa afanye hivyo ili wawe huru kwenye penzi lao. Wakati yote yanaendelea, Terry alikuwa bado yupo kwenye ndoa.
JOE WSTERMAN
February mwaka huu mchezaji huyu wa Rugby raia wa England alikamatwa kwenye kamera akiwa kwenye magahawa wa Greggs.
Joe alionekana akiwa anafanya vitendo visivyokuwa vya maadili na mwanamke mmoja kwene mgahawa huo hali iliyosababisha ugomvi mkubwa na mkewe Lauren, 33, baada ya video hiyo kusambaa hata akasababisha aondolewe kwenye nyumba ya familia aliyokuwa akiishi na mkewe na watoto wake.
Akizungumza kupitia tovuti ya The Sun Lauren alisema amekuwa akiiangalia video hiyo mara kwa mara na ameshindwa kabisa kufuta tukio hilo kwenye kichwa chake. Baadae Westerman aliomba msamaha na kudai kwamba ilikuwa ni akili ya pombe lakini hadi sasa bado hana uhusiano mzuri na mkewe aliyezaa naye watoto watatu.