Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachambuzi wanamuingiza Fei Toto kwenye chuki

Fei Toto Msh Wachambuzi wanamuingiza Fei Toto kwenye chuki

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lipo jambo hapa ambalo lazima tulizungumze, kuhusu mchezaji FEISAL SALUM na watu wa Yanga SC naamini wapo baadhi ya Wachambuzi wanamuingiza kwenye chuki bila ya yeye mwenyewe kujua.

Kwanza, YANGA ni taasisi ambayo ni kubwa nchini lakini siyo tu hapa nje ya mipaka yetu kwaiyo siyo rahisi kwa mtu mmoja kuweza kushindana na kundi la watu wote hao.

Kuondoka sehemu huwa haikatazwi lakini ukiendelea kutoa viashiria itaonekana ni kama una chuki na watu hao. Yanga SC ilivyomsajili Fei kutoka Singida hakuwa mchezaji maarufu lakini ukubwa wa Yanga ukampa jina mchezaji huyu na alipendwa sana ndani ya Klabu pale.

Hili la baadhi ya Wachambuzi kukaa kando yake na kuzitumia kalamu zao kama kumtengenezea mafuta na maji siyo kitu kizuri, wapo wenye uelewa kuwa hii ni kawaida lakini wapo wengi akili zao wanazijua mwenyewe, mimi nafikiri wengemuacha Feisal Salum acheze mpira bila ya kumtengenezea chuki kama hizo.

Yuko wapi BERNARD MORRISON ambaye naye alitengenezewa mambo kama hayo baadae ni kama ameuzika mpira wake. Kalamu zinaweza zikawa zinaandika lakini bila ya kutambua zinabomoa kwa kiasi kikubwa sana.

Ushauri wangu kwa FEISAL SALUM Ligi zimemalizika ni muda sasa wa yeye kujitenga na hao ambao ni kama wameamua kuzicheza vita zao na Yanga kupitia mgongo wake kwani asipokuwa makini watamuingiza katika maisha magumu ya soka. TANZANIA yetu wote hii kwaiyo tunatakiwa kuwa makini sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live