Mashabiki wa timu ya Yanga nchini Zambia, wamekerwa na tabia ya wachambuzi wa mpira miguu hapa nchini ya kuzipa hofu timu za ndani, kwa kuziongelea vibaya timu hizo, tofauti na wanavyoziongelea timu za wageni, huku wakiwataka wachambuzi hao kuiomba msamaha Yanga.
"Watu wanapenda kutembea na historia...lakini mpira wa miguu ni wa wazi na unaambatana pia na namna gani siku hiyo wachezaji wameamka, ukiwasikiliza wachambuzi hasa wa Tanzania...wa South Afrika nafikiri wachambuzi wao wako fair.
"Ukiwasikiliza wa Tanzania, kiukweli wanapaswa waiombe Yanga msamaha kwa sababu wao kama wananchi halisi wa Tanzania, hawakupaswa kuiongelea vibaya sana Yanga.
"Kwa sababu ukiangalia wengi...wote walikuwa wanaihofisha Yanga....unapomuongelea vizuri sana mgeni maana yake unamvunja moyo mwenyeji," Emmanuel Julius - Shabiki wa Yanga Lusaka Zambia.